Kufuatia uchakavu wa miundombinu ya majengo ya Chuo kikuu cha Mzumbe ambayo yalijengwa tangu mwaka 1953 kutokidhi viwango vya chuo hicho kwa sasa wanafunzi waliosoma chuoni hapo wakiwemo wadau wa elimu wamechukua hatua yakukihamisha na kujenga majengo ya kisasa yatakayo gharimu shilingi trilioni 1.4 na kukamilika ifikapo mwaka 2025.
Akizungumza na waandishi wa habari chuoni hapo Naibu Makamu Mkuu wa chuo hicho taaluma Josephat Itika amesema umoja wa wanafunzi waliosoma katika chuo hicho (Alumni) wakiwemo wadau wa elimu wameitisha kongamano la uchangishaji pesa ilikujenga majengo ya kisasa yanayo endana na hadhi ya chuo hicho .
Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof.Lughano Kusiluka amesema lengo la kongamano hilo la uchangiaji nikutaka kumwekea mazingira mazuri mtoto wa kike ambapo wameeleza mikakati ya kufanikisha ujenzi huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa ujenzi wa bweni la wasichana Juni 17 mwaka huu litakalo gharimu shilingi Bilioni 4.5 ambalo linatarajiwa kuingia zaidi ya wanafunzi mia tisa.