Friday, November 18, 2016

Videa ya Man Fongo awatoka BASATA baada ya kutaka kuufungia wimbo wake....,,

Image result for man fongo





Tazama Mwili wa msichana anayetarajia 'kufufuliwa'


Mchoro wa jinsi miili huenda ikahifadhiwa siku za usoniImage copyrightSCIENCE PHOTO LIBRARY
Image captionMchoro wa jinsi miili huenda ikahifadhiwa siku za usoni
Msichana ambaye alitaka mwili wake ugandishwe na kuhifadhiwa kwa matumaini kwamba anaweza kurejeshewa uhai wakati mmoja siku za usoni, alipata ushindi wa kihistoria saa chache baada ya kufariki dunia.
Msichana huyo alitaka mwili wake uhifadhiwe kwenye friji maalum baada ya kufa kwa matumaini kwamba anaweza kurejeshewa uhai, na hata ikiwezekana aponywe, baadaye. Mamake alimuunga mkono lakini babake alikuwa anapinga wazo hilo.
Msichana huyo mwenye umri wa miaka 14 alikuwa anaugua aina nadra sana ya saratani.
Jaji katika mahakama ya Uingereza aliamuru kuwa mama yake ndiye angekuwa na usemi wa mwisho kuhusu mwili wake.
Mwili wa msichana huyo, aliyefariki mwezi Oktoba, sasa umesafirishwa kwa ndege hadi Marekani kuhifadhiwa.
Msichana huyo alikuwa anaishi London na alitumia mtandao wa intaneti kusoma zaidi kuhusu teknolojia ya kuhifadhi miili ya cryonics miezi ya mwisho ya uhai wake.

Matumaini siku za usoni

Cryonics ni teknolojia inayotumia kuuhifadhi mwili kwa kuugandisha kwa matumaini kwamba huenda ikawezekana kuufufua au kupata tiba siku za usoni.
Msichana huyo alimwandikia jaji na kumwambia kwamba alitaka "kuishi muda mrefu" na hakutana "kuzikwa ardhini".
Freezing heart valves for preservationImage copyrightSCIENCE PHOTO LIBRARY
Aliandika: "Nafikiri kuhifadhiwa kwa teknolojia ya cryonic kutanipatia fursa ya kutibiwa na kuamshwa - hata kama ni baada ya miaka mia moja."
Jaji Justice Peter Jackson, alimtembelea msichana huyo hospitalini na anasema aliguswa sana na ujasiri ambao msichana huyo alikuwa nao katika kukabiliana na maradhi aliyokuwa anaugua.
Kwenye uamuzi wake, alisema, uamuzi huo haukuwa kuhusu usahihi au kutofaa kwa cyronics bali mzozo kati ya wazazi wa msichana huyo kuhusu hatima ya mwili wa binti yao.

Mwili kugandishwa

Cryonic ni shughuli ambayo imekuwa na utata mwingi na hakuna ajuaye iwapo inawezekana kufufua miili iliyogandishwa kufikia sasa.
Kuna vifaa Marekani na Urusi ambapo miili inaweza kuhifadhiwa kwenye madini ya naitorjeni kwenye baridi kali (chini ya nyozijoto -130C) - lakini huduma hiyo haipo Uingereza.
Gharama ya kugandisha mwili kwa muda usiojulikana inakadiriwa kuwa takriban £37,000.

Barua ya msichana kwa jaji

"Nimetakiwa kueleza ni kwa nini nataka jambo hili lisilo la kawaida lifanyike.
"Nina miaka 14 pekee na sitaki kufariki dunia lakini najua nitafariki dunia.
"Nafikiri kuhifadhiwa kwa njia hii ya cyronic kutanipa fursa ya kutibiwa na kuamshwa - hata kama ni miaka mia moja ijayo.
"Sitaki kuzikwa ardhini.
"Ninataka kuishi na niishi muda mrefu na nafikiri siku za usoni huenda kukapatikana tiba ya saratani ninayougua na kuniamsha.
"Ninataka kupata fursa hii.
"Hayo ndiyo mapenzi yangu.

Wazazi wa msichana huyo walitalakiana na msichana huyo hakuwa amekutana na babake kwa miaka sita kabla yake kuanza kuugua.
Mamake aliunga mkono mapenzi yake ya kutaka mwili wake uhifadhiwe kwa kugandishwa lakini babake alikuwa anapinga.
Babake alisema: "Hata kama itawezekana afufuliwe na atibiwe tuseme miaka 200 ijayo, huenda hatapata jamaa yeyote anayemjua na huenda asikumbuke mambo mengi. Atakuwa katika hali ya masikitiko ikizingatiwa kwamba ana miaka 14 na atakuwa Marekani."
Royal Courts of JusticeImage copyrightPA
Image captionKesi hiyo iliamuliwa na jaji wa Mahakama Kuu mjini London
Ingawa baadaye alibadili msimamo wake na kusema anaheshimu uamuzi wa bintiye, alitaka kuuona mwili wa bintiye baada ya kifo chake, jambo ambalo msichana huyo alikuwa amekataa.
Jaji alisema ombi la msichana huyo lilikuwa la kipekee kuwahi kuwasilishwa England na Wales, na labda kwingineko.

Kuhitajika kwa sheria

Jaji Jackson alisema kesi hiyo ni mfano wa matatizo mapya yanayoletwa na sayansi kwa wanasheria.
Msichana huyo alifariki Oktoba akifahamu kwamba mwili wake ungegandishwa, lakini jaji alisema kulikuwa na matatizo siku aliyofariki.
Wahudumu wa hospitali na wakuu wao walieleza wasiwasi kuhusu jinsi mwili wake uliandaliwa kwa ajili ya kuhifadhiwa.
Hilo lilifanywa na kundi la watu wa kujitolea Uingereza kabla ya mwili huo kupelekwa Marekani.
Amedokeza kwamba mawaziri wanafaa kutafakari uwezekano wa kutoa kanuni na sheria za kusimamia uhifadhi wa miili kwa kutumia teknolojia ya cyronic siku za usoni.


CHANZO; BBC

Wednesday, November 16, 2016

Mjenga misuli ala kondo la nyuma la mpenziwe...


Wajenga misuli, AustraliaImage copyrightAP
Image captionWajenga misuli, Australia
Mjenga misuli ambaye alipata umaarufu kwenye mtandao baada ya kuchoma na kula kondo la nyuma la mpenzi wake amesema kondo hiyo lililokuwa kama maini.
Mwamume huyo mwenye umri wa miaka 32 kutoka Australia amesema atakuwa 'makini' jinsi kondo hiyo ingeonja.
''Mpenzi wangu hakuwa na shida nami kula nyama hiyo, lakini nilipoianza kuichoma jikoni , sidhani alipenda,Aaron Curtis amesema.
''Haikuwa na ladha tofauti lakini ngozi yake ilinikumbusha maini.''
Wakati wa uja uzito , kondo la nyuma husambaza chakula kutoka kwa mama hadi kwa mtoto.
Kwa mzazi kula kondo hiyo, baada ya kujifungua , si jambo la kushangaza kwamba kondo hiyo ina virutubisho vya kiasili.
Nimekuwa na maoni tofauti kuhusiana na kutupa chakula , kwa hivyo ulaji wa kondo hiyo halikuwa jambo kubwa kwake , amesema Aaron.
Nimekuwa na wiki nzuri katika mazoezi yangu baada ya kula kondo hiyo igwaje usingizi wangu umekuwa ukitatizwa na jukumu la ubadilishaji nepi.


CHANZO; BBC

Friday, October 21, 2016

Teknomiles - Diana [Official Video].....


New Video Teknomiles-Diana

Nguli wa muziki wa afro jazz Kenya Achieng Abura afariki dunia...



Achieng AburaImage copyrightACHIENG ABURA / FACEBOOK
Image captionAchieng Abura alishinda tuzo ya Kora mwaka 2004

Mwanamuziki nguli wa nyimbo za mtindo wa Afro Jazz kutoka Kenya Achieng Abura amefariki dunia.
Mwanamuziki huyo aliaga dunia akipokea matibabu katika hospitali kuu ya taifa ya Kenyatta (KNH) jijini Nairobi.
Lydia Achieng Abura, alipata umaarufu miaka ya 1990 kwa wimbo wa injili kwa jina I Believe.
Baadaye, alianza kukumbatia mitindo mingine ya uimbaji kama vile jazz.
Kwenye ujumbe katika ukurasa wa Facebook mapema mwezi huu, alikuwa amedokeza kwamba hakuwa buheri wa afya.
Alisema alikuwa amepoteza uzani wa kilo 50 katika kipindi cha miaka mitatu pekee, na madaktari walikuwa wamemshauri kuongeza uzani.
"Kutembea ni shida na ninaumwa kila pahali," aliandika.

Achieng AburaImage copyrightACHIENG ABURA / FACEBOOK

Kwenye mahojiano na gazeti la Business Daily mwezi Julai, alikuwa amesema alikabiliwa na matatizo ya kifedha kutokana na afya ya mwanawe wa kiume aliyehitaji kufanyiwa matibabu ambayo yangegharimu Sh4 milioni (dola 400,000 za Marekani).
"Niliandaa mchango lakini waliohudhuria walikuwa chini ya 10," aliambia gazeti hilo.
Abura alishinda tuzo ya muziki ya Kora mwaka 2004.
Alikuwa pia jaji katika shindano la kuwatafuta wanamuziki wenye vipaji la Tusker Project Fame ambalo liliwashirikisha vijana kutoka nchi za Afrika Mashariki.
Wanamuziki wenzake, viongozi na mashabiki wameeleza kushangazwa kwao na kifo hicho na wamekuwa wakituma salamu za rambirambi mtandaoni.

Suzanna OwiyoImage copyrightTWITTER
Sauti SolImage copyrightTWITTER

AliKiba na Mr Blue waungana kwajili ya Abby Skills.....

Msanii ambaye alifanya vizuri kipindi cha nyuma na nyimbo ‘Maria’ na ‘Mimi na Wewe’ Abby Skills anajipanga kurudi upya katika game la muziki na wimbo ‘Averina’ akiwa na Ali Kiba.
Image result for alikiba na mr. blue
Muimbaji huyo ameiambia Bongo5 kuwa AliKiba na Mr Blue ndiyo watu ambao wanamsimia kwa sasa ili kumrudisha upya kwenye chati.
“AliKiba na Mr Blue walikaa chini na kuamua kunisaidia kunirudisha kwenye game,” alisema Abby. “Waliniambia tumeona una kipaji kizuri, una melody ngoja tushirikiane ili kukupeleke sehemu fulani,”
Aliongeza, “Hata hii project yangu mpya na AliKiba ‘Averina’ wao ndio wanasimamia kila kitu, kwa hiyo kuna mambo mazuri yanakuja hivi karibuni,”
Muimbaji huyo amesema kazi yake mpya aliyomshirikisha AliKiba itatoka hivi karibuni kwa kuwa tayari ameshashoot na video.

Thursday, October 20, 2016

MBWA ALIYE DUNGWA MSUMARI KICHWANI LAKINI AWA HAI....


Mbwa azikwa akiwa hai huku akiwa amedungwa msumari kichwani
Image captionMbwa azikwa akiwa hai huku akiwa amedungwa msumari kichwani
Mbwa mmoja amepatikana amezikwa akiwa hai huku msumari ukiwa umedungwa kichwani mwake katika eneo la Teesside katika kile shirika linalokabiliana na unyanyasaji wa wanyama nchini Uingereza RSPCA linasema ni kitendo cha ukatili.
Wanandoa wawili waliokuwa wakitembea katika eneo la Kirkleatham Wood ,walisikia kilio cha kitu kilichokuwa kikilia kwa uchungu na kumpata mbwa huyo ambaye tayari alikuwa amezikwa.
Alikimbizwa kwa daktari wa wanyama lakini majeraha yake mabaya yalimlazimu mtabibu huyo kumuua.
Shirika hilo la wanyama linasema kuwa zaidi ya mtu mmoja alihusika katika kitendo hicho.
Inspekta Nick Jones alisema: katika kipindi cha miaka kumi ambacho nimefanyia kazi RSPCA,sijawahi kuona kitu cha kuogofya na ukatili mkubwa kama huu.

Sunday, October 2, 2016

Yaliyotokea siku kama ya leo katika historia duniani tarehe 02 octoba.....



Siku kama ya leo miaka 147 iliyopita, alizaliwa Mahatma Gandhi, kiongozi wa harakati ya kupigania uhuru nchini India katika moja ya vijiji vya jimbo la Gujarat. Mwaka 1891.Gandhi alirejea kutoka nchini Uingereza na kuishi mjini Mumbai. Mwaka 1893 Mahatma Gandhi alielekea mjini KwaZulu-Natal nchini Afrika Kusini. Akiwa nchini humo alishuhudia ubaguzi wa rangi wa jamii ya wachache ndani ya taifa hilo. Mwaka 1917 na baada ya kurejea nchini kwake alipata umashuhuri mkubwa. Na miaka michache baada ya Vita vya Kwanza na vya Pili vya Dunia yaani akiwa na umri wa miaka 33 aliongoza mapambano kwa ajili ya kuwaokoa watu wake sanjari na kupigania uhuru wa India kutoka mikononi mwa Waingereza ambapo hatimaye na baada ya kuvumilia matatizo mengi tofauti kama vile Jawaharlal Nehru akafanikiwa kulipatia uhuru taifa hilo hapo mwaka 1947.
Siku kama ya leo miaka 112 iliyopita sawa na tarehe Pili Oktoba 1904, alizaliwa Graham Greene mwandishi wa Uingereza. Siku zote mwandishi huyo aliakisi matendo mema na mabaya katika athari zake na aliandika kwenye kitabu chake kinachoitwa 'Nguvu na Utukufu' kwamba subira, uvumilivu na mateso ni njia ya wokovu. Graham Greene ameacha vitabu vingi ambapo baadhi ni 'Mtu wa Tatu', 'Utawala Unaotisha' na Muuaji wa Kukodishwa'. Mwandishi huyo Muingereza alifariki dunia mwaka 1991.
Siku kama ya leo miaka 58 iliyopita yaani sawa na tarehe Pili Oktoba 1958, nchi ya Guinea Conakry ilifanikiwa kujipatia uhuru wake kutoka kwa mkoloni Mfaransa. Wareno walianza kumiminika nchini Guinea mwishoni mwa karne ya 15, na ilipoanza karne ya 19, Wafaransa wakawa na satua zaidi nchini humo na ulipotimia mwaka 1849, nchi hiyo ikakoloniwa rasmi na Ufaransa. Guinea Conakry inapakana na nchi za Senegal, Mali, Ivory Coast, Liberia, Sierra Leone na Guinea Bissau.

NEW VIDEO; LADY JAY DEE - SAWA NA WAO [music]


LADY JAY DEE - SAWA NA WAO [music video/audio]

Tuesday, September 27, 2016

Mwinjilisti ajinyonga hadi kufa baada ya kumuua mwanaye kwa madai alikuwa anafanya ufuska...

Mwinjilisti wa Kanisa la African Inland Church (AICT), Charles Kazereng’wa (45), amejinyonga hadi kufa, baada ya kumuua mwanaye, Malita Charles (15) kwa kumpiga akimtuhumu kujihusisha na ufuska
Image result for kitanzi

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Geita, Mponjoli Rodson amelithibitishia gazeti hili kutokea kwa matukio hayo juzi jioni.
Hata hivyo, alisema kuwa asingeweza kulizungumzia suala hilo kwa undani kwa sababu alikuwa kwenye sherehe za uzinduzi wa Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo kitaifa inafanyika mkoani Geita.
Hata hivyo, habari za uhakika kutoka katika Kitongoji cha Elimu, Kijiji cha Kaseme kilichopo wilayani Geita ambako mwinjilisti huyo alikuwa akiishi na familia yake zinasema kuwa alichukua uamuzi wa kumwadhibu binti yake huyo aliyehitimu darasa la saba mwaka huu, baada ya kumkuta akizungumza na mwanamume ambaye hata hivyo hakufahamika.
Inaelezwa kuwa baada ya kumpiga, alimchukua na kwenda naye nyumbani na kumfungia ndani huku akiendelea kumwadhibu hadi alipofikwa na umauti.
Kwa mujibu wa shuhuda ambaye hakuwa tayari kutajwa jina gazetini, baada ya mwinjilisti huyo kubaini kuwa amemuua mwanaye, alichukua uamuzi wa kukimbia umbali ya kilometa moja na kujitundika mtini kwa kamba iliyomnyonga hadi kufa.
Kamanda Mponjoli, alisema kuwa uchunguzi wa Polisi na wa madaktari unaendelea na kwamba utakapokamilika miili ya marehemu wote wawili itakabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya maziko.
Aliitaka jamii kuwa makini wakati wa kuadhibu watoto kwa kuwa si wakati wote wanapaswa kupewa adhabu kali na hatarishi kama vipigo vinavyoweza kuwasababishia umauti.
Wakati huohuo, baadhi ya wakazi wa Kata ya Kaseme wanaomfahamu mwinjilisti huyo walieleza kwa nyakati tofauti kushangazwa na hatua aliyoichukua kwa sababu hakuwa na tabia ya uhalifu wa aina yoyote wala ukatili.
Masaga Makanika na Magesa Masai kila mmoja kwa wakati wake alisema kuwa mwinjilisti huyo alikuwa ni muumini mzuri wa dini asiye na rekodi mbaya ya matukio ya kiuhalifu na kwamba hatua alizochukua zimewaacha na maswali mengi huku wakifikiri kuwa pengine ni mipango ya Mungu au majaribu ya shetani.

Source: Habari Leo

Huyu ndiye staa aliyeweka rekodi ya kufikisha followers milioni 100 kwenye Instagram.....

Selena Gomez amekuwa staa wa kwanza duniani kufikisha idadi ya followers milioni 100 kwenye mtandao wa Instagram.
selena
Kwa mara ya kwanza Selena alimnyang’anya taji hilo Taylor Swift mwezi Machi mwaka huu baada ya kufikisha followers milioni 69.7 wakati huo Taylor akiwa na followers 69.3m.
img-20160925-wa0007-1
Na sasa nafasi ya pili inashikiliwa na T-Swift mwenye followers milioni 91.4, Beyonce milioni 85.5m, Kim Kardashian 83.6m.

NEW VIDEO; Msami baby – Step by step (OFFICIAL VIDEO)....

Msanii wa bongo fleva Msami baby ambaye ni mkali wa ku Dance, ameachia hii video mpya ya wimbo wake wa “Step by step”, video imeongozwa na Khalfan.

Friday, September 23, 2016

Staa wa Nigeria Chinedu Ikedieze (Aki) afunguka kuhusu ‘Salome’ ya Diamond ‘I am a big fan’....

chinedu-1

Salome ya Diamond Platnumz inaelekea kumshangaza staa huyo kwa mafanikio makubwa inayoendelea kuyakusanya.


Baada ya video yake kuvutia views milioni 1 ndani ya siku mbili tu tangu itoke, wimbo huyo umeyagusa masikio ya mtu maarufu kwenye filamu za Nigeria, Chinedu Ikedieze anayejulikana zaidi kama Aki kwenye filamu zake.
Image result for AKI


Akicomment kwenye post ya Diamond Instagram, Ikedieze amesema kuwa haelewi kinachoimbwa kwenye wimbo huo lakini ameupenda na kwamba ni shabiki wake mkubwa.
cs-oiyxgaa7hye
chinedu
Aki na Ukwa wamekuwa na mashabiki wengi Afrika nzima kwa filamu zao za comedy.

Wenger: Sitasoma kitabu cha Mourinho.....



Image captionImage result for wenger and mourinhoArsene Wenger na Jose Mourinho wakizozana awali

Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger anasema kuwa ''hatosoma'' kitabu ambacho mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho amesema atauvunja uso wa kocha huyo wa Arsenal.
Mourinho amekuwa akizozana na Wenger alipokuwa akiifunza Chelsea na alimuita mkufunzi huyo ''maalum kwa kushindwa''.
''Mimi huzungumza kuhusu soka-hicho ndio ninachofanya'',alisema Wenger mwenye umri wa miaka 66.
''Siko katika hali ya kutaka kuharibu,mimi hupenda kujenga.Ninaangazia mechi ya Jumamosi dhidi ya Chelsea''.
Mourinho mwenye umri wa miaka 53 alimuita Wenger ''mpiga chabo'' mwaka 2005 baada ya kutaka kujua kuhusu sera za uhamisho za Chelsea.
Raia huyo wa Ureno alimuita Arsene Wenger ''mtu maalum kwa kushindwa'',mnamo mwezi Februari 2014 baada ya raia huyo wa Ufaransa kusema kuwa baadhi ya wakufunzi wa ligi kuu ya Uingereza wameanza kulalamika kwa sababu ''wanahofia kufeli''.
Image result for wenger and mourinho

Mtoto wa miaka 6 amuandikia Rais Obama barua kuhusu mtoto Omran wa Syria aliyeokolewa...



Picha ya Omran Daqdees mwenye miaka mitano ambayo alionekana akiwa na vumbi na damu baada ya nyumba yao huko Aleppo Syria kuharibiwa katika mlipuko, picha hiyo iliwashtua wengi duniani mwezi uliopita ikiwa ni pamoja na mvulana aitwaye Alex, ambaye anaishi Scarsdale, New York. Alex imembidi amwandikie barua President Obama ikiwa na mstari unaosema ‘atakuwa mwanafamilia mwenzetu na atakuwa kaka yetu’
Baada ya kupokea barua hiyo Rais Obama ameishare video kwenye ukurasa wake wa facebook  yenye barua hiyo na kuandika hivi…………
>>>Alex ni mtoto mwenye miaka sita. Anaishi Scarsdale, New York Marekani, mwezi uliopita kama watu wengine duniani aliguswa na taarifa za picha za mtoto Omran Daqneesh, mwenye umri wa miaka mitano huko Aleppo Syria, aliyekuwa amekaa kwenye gari la wagonjwa (Ambulance) akiwa na taharuki huku akijaribu kujifuta damu mikononi mwake.
>>>Hivyo Alex alikaa chini na kuniandikia barua, wiki hii katika mkutano wa Umoja wa mataifa uliokuwa ukijadili masuala ya wakimbizi, niliishirikisha dunia maneno mazito ya Alex.
>>>Alex aliniambia alitaka Omran aende kuishi naye pamoja na familia yake, alitamani atumie naye baisikeli yake, pia amfundishe jinsi ya kuiendesha. Akasema dada yake atakuwa akimkusanyia vipepeo, na watakuwa wakicheza wote pamoja, akaandika “Tutamfanya familia na atakua kaka yetu.
>>>Hayo ni maneno ya mtoto wa miaka sita ambaye bado hajajifunza kutuhumu au kuwa na wasiwasi na woga kwa watu wengine kulingana na walipotoka, wanavyoonekana ama jinsi wanavyo abudu.
>>>Inabidi nasi  tuwe kama Alex, fikiria dunia ingekuwaje kama tungekua kama yeye. Tafakari tugepunguza maumivu kiasi gani na tungeokoa maisha ya watu wangapi. Msikilize Alex, soma barua yake, na ninafikiri utanielewa kwanini niliushirikisha ujumbe huu kwa dunia. 

38b547a600000578-3803449-image-m-197_1474609204984

38b547b000000578-3803449-image-m-196_1474609190097
38b547b900000578-3803449-image-m-195_1474609175705



Nyoka atafuta' joto' kwenye kiatu Australia.....


Nyoka mwenye sumu kali atafuta 'joto' kwenye kiastu AustraliaImage copyrightSNAKE CATCHERS ADELAIDE
Image captionNyoka mwenye sumu kali atafuta 'joto' kwenye kiastu Australia

Mwanamke wa Australia amewaita maafisa wa wanyama pori kumtoa nyoka wa urefu wa mita 1 mwenye sumu kali kutoka kwenye kiatu chake.
Mnasa nyoka Rolly Burrell alimdhibiti nyoka huyo wa rangi ya chokoleti aliyekuwa anatafuta ''joto'' nyumbani mwa mwanamke huyo Adelaide, kusini mwa Australia.
Alikuwa ametoka nje ya nyumba yake iliopo mashambani kukusanya viatu vyake na hapo akaona mkia ukipotea ndani ya kiatu chake kimoja.
Nyoka huyo ni mmoja wa wanaoonekana kuwa wenye sumu kali duniani na hupatikana katika pwani na maeneo ya ndani ya ardhi kavu Australia.


"Alitoka nje kuchukua viatu vyake na akaona kitu kikitoweka kwa kasi," Burrell ameiambia BBC.
"Aligundua kuwa ni nyoka."
Nyoka huyo ambaye ni aina inayopenda kujificha, alichiliwa msituni kando na mbali na maenoe ya makaazi ya watu .
Bwana Burrell amesema kampuni yake iliitwa kwa mara nyengine kutoa nyoka kwenye kiatu takribana mwaka mmoja uliopita.
Viatu hivyo aina ya buti, vimetengenezwa kwa ngozi ya kondoo, na hutumika sana Australia, Huwana joto zuri wakati wa msimu wa baridi, pengine ndio sababu iliomvutia nyoka huyo.
"Ndio wanaanza kuamka kutoka usingizini," Bwana Burrell anasema.
"Msimu wao wa kujamiiana umeanza kwa hivyo wanatafuta joto na wana njaa.



CHANZO:BBC

NEW VIDEO; JUMA NATURE - MTUMBA...

Image result for JUMA NATURE - MTUMBA


     Angalia Video hii yapa...
     Watch Video here....

NEW FILM; Kenneth smith - English Action Movies Full New Hollywood Movies 2016


Best Action Sci fi Movies 2016 - English Action Movies Full New Hollywood Movies 2016

WCB WASAFI GIZANI na Diamond Platnumz....

kumbe sio sisi tu hata nawao WCB wasafiiiiiii.....

Waziri Kindamba ateuliwa kuwa Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL....

TTCL imepata bosi kijana, Waziri Waziri Kindamba.
dsc_5652
Uteuzi huo uliofanywa na Rais John Magufuli, umetangazwa Ijumaa hii.
ctbmz7yweaa2rlt
Kupitia blog yake, Kindamba anajielezea kama: ni mhitimu wa shahada ya Uzamili katika Uongozi wa Biashara na Shahada ya Benki, Uchumi na Sheria) mwenye ujuzi wa Teknohama na uwezo mkubwa wa kujenga uhusiano aliye tayari kukabaliana na changamoto na kuzitumia fursa zilizopo jimboni . Mwenye uwezo wa kufanya kazi mahali popote aliye na ufahamu wa hali ya juu wa masuala ya Benki, Uchumi, Benki na Sheria za Biashara, Fedha na Stadi za Maendeleo.