Saturday, March 11, 2017

Top 10 ya viwanja vya ndege vilivyokuwa busy zaidi duniani 2016....


Rekodi mbalimbali zimewekwa katika mambo mengi Duniani kuanzia michezo, sanaa, magari, nyumba, hotel na mengine huku wahusika wakijitahidi pia kujiweka tayari kuzilinda rekodi hizo.
Leo March 10 2017 vimetajwa viwanja vya ndege ambavyo vilioongoza kwa kuwa busy zaidi duniani mwaka 2016 ambapo Hartsfield-Jackson Atlanta International Airport kimeongoza kwa abiria milioni 104 waliofanya safari zao kupitia uwanja huo ikiwa ni mara ya 19 mfululizo.
10: Paris-Charles De Gaulle Airport, France
Unakamata nafasi ya 10 katika list hii baada ya kuhudumia abiria zaidi ya milioni 66 mwaka 2016.
9: Shanghai Pudong International Airport, China
Zaidi ya abiria milioni 66 mwaka 2016 ambao ni ongezeko la 10%.
8: Hong Kong International Airport, China
Hong Kong inakamata nafasi ya nane kwa kuhudumia abiria zaidi ya milioni 70 mwaka 2016.
7: London Heathrow Airport, United Kingdom
Abiria wanaotumia Heathrow waliongezeka kwa 1% na kufanya zaidi ya milioni 75 mwaka 2016 hivyo kuuangushia nafasi ya saba kutoka sita mwaka uliopita.
6: Chicago’s O’Hare International Airport, United States
Uwanja mkubwa zaidi mjini Chicago ulihudumia abiria zaidi ya milioni 78 mwaka 2016 ongezeko la 2%.
5: Tokyo’s Haneda International Airport, Japan
Zaidi ya abiria milioni 79 mwaka 2016 ongezeko la 6% wanaifanya Haneda kukamata nafasi ya tano.
4: Los Angeles International Airport, United States
Uwanja maarufu zaidi Southern California ulisafirisha abiria milioni 81 mwaka 2016, 8% zaidi ya 2015.
3: Dubai International Airport, United Arab Emirates
Uwanja uliokuwa busy zaidi Middle East, Dubai ulihudumia abiria zaidi ya milioni 83 mwaka 2016, zaidi ya 7% ukilinganisha na 2015.
2: Beijing Capital International Airport, China
Ukihudumia zaidi ya abiria 94 million mwaka 2016, ongezeko la 5%, Beijing umeendelea kuifukuzia namba 1.
1: Hartsfield-Jackson Atlanta International Airport, USA
Ulikuwa busy zaidi duniani mwaka 2016 ukihudumia zaidi ya abiria milioni 104 mwaka 2016 ongezeko la 3%.

No comments:

Post a Comment