Thursday, March 16, 2017

G Nako akana kuicopy ‘Go Low’ ya FlowKing Stone wa Ghana...

Go Low’ ni ngoma mpya ya G Nako na Jux ambayo imepikwa na mpishi wa mziki anayefanya vizuri nchini kwa sasa King Luffa licha ya ngoma hiyo kufanana Chorus na ngoma ya FlowKing wa Ghana.
Kwa upande wangu kila nikisikiliza ‘Go Low’ ya kibongo na ya Flow King wa Ghana nikifika kwenye Chorus naona hakuna utofauti kabisa nikahisi labda kuna kitu kimejificha tusichokijua kutoka kwa G na huyo mjamaa. Nimemtafuta G Nako amegoma kuicopy ngoma hiyo iliyotoka August mwaka jana na Ilifanya vizuri sana huko Ghana.
“Inatokeaga nyimbo kufanana na sio kitu cha ajabu sana unajua, lakini mimi before nilikuwa sijafahamu nimekuja kujua baada ya kuitoa hiyo kazi,” ameyasema kupitia kipindi cha Zero Planet cha Ice Fm. “Mi uwa nacreate idea zangu lakni nahisi imetokea tu bahati mbaya idea kama zimefanana hivi,” ameongeza
Alipoulizwa kama idea ametoka nayo home au aliikuta studio, G amesema, “biti niliikuta studio na hiyo kazi imetengenezwa studio na hiyo kazi sisi tumeitengeneza mwaka jana na video tumeshoot mwezi wa tisa.
Go Low ya Ghana ilifanya vizuri zaidi pale FlowKing Stone alipofanya remix ya ngoma hiyo kwa kuwakutanisha wakali kibao kama Stonebwoy, Edem, D Black, Teephlow, Gasmilla, Francy na Gadam.


Hata hivyo G Nako amewalaani vikali wabadhilifu wa kazi za wasanii ambao wanachukua kazi za wasanii na kuzisambaza kinyemela hali kwa sasa kuna mitandao special kwa kuwasapoti wasanii.

No comments:

Post a Comment