Monday, March 6, 2017

Yaliyotokea siku kama ya leo kihistoria duniani Machi 1....



Siku kama ya leo miaka 202 iliyopita yaani mwaka 1815, ufalme wa siku mia moja wa Napoléon Bonaparte ulianza nchini Ufaransa baada ya kukimbia sehemu aliyokuwa amebaidishiwa katika kisiwa cha Elba. Napoleon Bonaparte tarehe 27 mwezi Februari mwaka huohuo akiwa pamoja na wanajeshi elfu moja alifanikiwa kutoroka katika kisiwa cha Elba ambapo alikaa humo akiwa uhamishoni kwa kipindi cha miezi kumi na kurejea Ufaransa. Hivyo utawala wa kifalme ulianza huko Ufaransa baada ya Napoleon kuwasili nchini humo.
Siku kama ya leo miaka 125 iliyopita yaani tarehe 1 Machi mwaka 1892 alizaliwa mjini Tokyo mwandishi na mtaalamu mkubwa wa fasihi wa Japan, Rhunosuke Akutagawa. Mwandishi huyo anahesabika kuwa ni mmoja wa waasisi wa kanuni mpya za fasihi nchini Japan. Akutagawa ameandika vitabu muhimu kama "Binti wa Buibui" na "Tushi Gun." Mwandishi huyo alifariki dunia mwaka 1927.
Na miaka 119 iliyopita siku kama leo, kisiwa cha Puerto Rico kilichoko katika ya Bahari ya Atlantic kaskazini mwa Amerika ya Kusini, kilikaliwa kwa mabavu na vikosi vya Marekani baada ya kumalizika vita vya kikoloni vya Uhispania na Marekani. Baada ya Marekani kukitwaa kwa nguvu kisiwa hicho ilikifanya ghala kubwa la silaha, kiasi kwamba Marekani iliasisi kambi 13 za kijeshi kisiwani humo. Kisiwa hicho ambacho mara kwa mara hukumbwa na ukosefu wa amani, ni ardhi iliyoko Amerika inayotumia lugha ya Kihispania

No comments:

Post a Comment