Wednesday, March 1, 2017

LG yazindua simu mpya yenye skrini mbili,Tazama picha za simuhiyo....

Kampuni ya LG yazindua simu mpya yenye skrini mbili


LG G6 ina rangi aina tatuHaki miliki ya pichaLG
Image captionLG G6 ina rangi aina tatu

LG imezindua simu mya ambayo skrini yake ni kubwa na ambayo inaweza kutumiwa njia tofauti kwa wakati mmoja.
Simu hiyo LG G6 ina mfumo wa 18:9 badala ya mfumo wa 16:9 ambao unatumiwa na simu nyingi.
Hii ina maana kuwa skrini hiyo inaonekana kubwa kuliko kawaida.
LG imekiri kuwa simu iliyozinduwa awali ya G5 ilishindwa kufikia malengo yake ya mauzo.

LG inasema kwa simu hiyo haiwezi kuathiriwa na maji wala vumbiHaki miliki ya pichaLG
Image captionLG inasema kwa simu hiyo haiwezi kuathiriwa na maji wala vumbi

Simu hiyo ilizinduliwa mjini Barcelona kabla ya kuanza kwa mkutano wa simu za mkononi duniani.
Skrini ya LG G6 ina upana wa sentimita 14.5 ikilinganishwa na skrini ya sentimita 13.5 ya LG5.
Simu hiyo mya pia inawewa kuzamishwa ndani ya maji hadi muda wa nusu saa bila ya kukumbwa na tatizo lolote.

Skrini hiyo imetengenezwa kuonyesa sehemu mbili wakati mmoja
Image captionSkrini hiyo imetengenezwa kuonyesa sehemu mbili wakati mmoja
G6 ni ndogo kuliko G5 lakini skrini yake ni kubwaHaki miliki ya pichaLG
Image captionG6 ni ndogo kuliko G5 lakini skrini yake ni kubwa

No comments:

Post a Comment