Monday, March 6, 2017

wasanii wa hip hop ni wabinafsi adai Madee....

Baada ya wiki iliyopita Madee kudai muziki wa hip hop Bongo kwa sasa umepooza, rapper huyo amekuja ni lingine kwa wasanii wa muziki huo.
Image result for madee
Madee amekiambia kipindi cha Dj Show cha Radio One kuwa wasanii wa hip hop wamekuwa wabinafsi wa kupeana connection za nje wanapozipata.
“Mimi kwa mtazamo wangu ambacho nakiona kimemiss kwenye muziki wa hip hop/rap ni connection ambazo sisi wenyewe tumekuwa tunazificha. Unakuta mtu kafanikisha kutoboa nchi fulani sasa atataka asurvive yeye kama yeye peke yake wakati hauwezi kufanikiwa kama hauna hauna ushirikiano na watu wengine nyuma ya pazia,” amesema Madee.
“Kwahiyo mwisho wa siku unahangaika na nafasi yako itaenda itaisha basi utaona umeshafanikisha lakini kumbe ungekuwa na wenzio kungekuwa na nguvu kubwa tofauti na hiyo moja ambayo uliyokuwa nayo wewe,” ameongeza.
“Connection ndio kitu kikubwa tumekuwa hatuna, jealous zimekuwa nyingi kwa wanamuziki wa hip hop huwa hawana ushirikiano wa kihivyo yaani,” amesisitiza.

No comments:

Post a Comment