Tuesday, August 30, 2016

80 WANUSURIKA KUTEKETEA KWA MOTO MKOANI MANYARA.......




Headlines za baadhi ya mabweni ya shule kuungua katika mkoa wa Arusha na manyara imekuwa ikiendelea ambapo katika mkoa wa Arusha jeshi la  polisi kupitia kwa kamanda Charles Mkumbo aliviambia vyombo vya habari kwamba kwa Arusha mpaka sasa hivi ni mabweni ya shule sita  ndio yaliyoungua.
Image result for manyaraImage result for manyara
Aidha idadi ya shule ambazo zinakuwa zimekumbwa na matukio hayo iliongezeka Jana August 29 2016 ambapo bweni la shule ya Aldasgate wilayani babati mkoani manyara limeungua, tukio hilo limekuwa ni la pili kwa mkoa wa manyara. Kamanda wa polisi Manyara Fransis Jacob amesema……….
>>>’Bweni moja liliwaka moto na hivyo kuteketeza baadhi ya vitu vya wanafunzi lakini kwenye vyumba hivyo viliweza kuokolewa lakini baadhi, kama asilimia 80 ya vitu viliweza kuokolewa, bado tunafanya uchunguzi kujua chanzo chake’
Tukio hilo la shule ya Aldasgate linafanya matukio ya kuungua kwa shule kwa kanda ya kaskazini kufikia nane ndani ya kipindi kifupi.

NAHREEL: AMWAGA SUMU MPYA THE INDUSTRY...


2
Mtaarishaji bora wa music nchini Tanzania 2015-2016 EMMANUEL MKONO Maarufu kama NAHREEL sasa yupo mbioni kuibua vipaji vipya katika tasnia hiyo ya utaarishaji wa muziki Nchini Tanzania.
Mtaalishaji huyo ambaye pia ni  C.E.O wa Label ya The industry Tz amesema hayo mara baada ya kuwasili jana siku ya jumatatu ktk makazi yake jijini Dar es salaam kutoka katika moja ya tour za fiesta zinazoendelea katika mikoa tofauti nchini Tanzania
“Mmmh nafikiri ni mapema sana kuzungumzia hilo ila!!!! Yaah kuna watu ninao tayari na tayari tameanza kuealekezana vitu vichache kuhusu production,walikuja wengi,   zaidi ya  ishirini lakini tukaangalia wale ambao tunaweza kuwa nao na kuelekezana vitu vichache tu but now nipo na hiyo project na nta introduce itapofika wakati soon” alisema Nahreel
Pia amewakumbusha mashabiki wa navy kenzo na The industry kwa ujumla kuwa sasa wanaweza kupata taarifa za label hiyo kwa kudownload APP TIMA (The Industry Music App) ambayo itawasaidia kupata taarifa za kipekee


VIDEO: Jah Prayzah asherehekea Watora Mari kufikisha views mil 1 ndani ya wiki 2.....

Jah Prayzah amesherehekea baada ya video ya wimbo wake wa ‘Watora Mari’ aliomshirikisha Diamond kufikisha views milioni moja kwenye mtandao wa Youtube.
Jah-1
Wimbo huo una wiki mbili tangu umewekwa kwenye mtandao huo August 12, mwaka huu lakini pia ndio wimbo wa kwanza wa msanii huyo kutazamwa mara nyingi kama hivyo.
Kupitia mtandao wa Instagram msanii huyo amewashukuru mashabiki wake kwa kuandika, “Thanks to all my fans out there,watora mari video with @diamondplatnumz has just reached a million views in a space of 2 weeks…”Aidha kwa mara ya kwanza wimbo huo utaanza kuchezwa leo kwenye runinga ya MTV Base.
Tazama video ya Jah Prayzah akisherehekea na rafiki zake kwa kufikisha views milioni 1.

Sheria tata za mtindo wa nywele katika shule za sekondari Africa.Kusini zasitishwa


Image captionMaandamano ya wanafunziWanafunzi katika shule ya sekondari ya Pretoria wanasema kuwa mara kwa mara waalimu huwaambia wanyooshe nywele zao na hawaruhusiwi kuzitengeneza katika mtindo wa Afro.
Sheria kuhusu namna wasichana wa shule za sekondari wanavyochana nywele nchini Afrika Kusini zimesitishwa baada ya maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi yaliyofanywa na wanafunzi weusi, ameleza waziri nchini humo.
Wanafunzi katika shule ya sekondari ya Pretoria wanasema kuwa mara kwa mara waalimu huwaambia wanyooshe nywele zao na hawaruhusiwi kuzitengeneza katika mtindo wa Afro.
Picha za mwanafunzi wa kike aliyeandamana kupinga sheria hiyo iliibua mjadala mkali kwenye mitandao ya kijamii kuhusu ubaguzi, ambapo #AchaUbaguziKatikaPretoriaGirlsHigh ilitumiwa na watu zaidi ya mara 150,000 kwenye mtandao wa Twitter.
Maandamano ya wanafunziImage copyrightTWITTER/@SIMAKELED
Image captionPicha ya mmoja wa waandamanaji iliyosambazwa kwa maelfu ya watu kwenye Twitter
Sheria za shule zitasitishwa huku uchunguzi huru ukifanyika kuhusiana na madai hayo, amesema waziri wa elimu katika mkoa wa Gauteng.
Shule ya sekondari haijatoa kauli yoyote.
Kanuni kuhusu maadili ya shule hiyo ina orodha ya sheria kuhusu nywele, lakini haijataja mtindo wa nywele wa afro.

VIDEO: Ariana Grande Feat. Nicki Minaj – Side to Side

WATCH  HOT VIDEO..
Fresh off her performance with Nicki Minaj at the VMAs, Ariana Grande unleashes the steamy video for “Side to Side.”
In the Hannah Lux Davis-directed clip, the pop princess echoes the fitness theme of her live rendition, setting it off by spinning with a team of dancers in a pink workout outfit and a hat that reads “Icon.” She hits the locker room for the second verse of the Caribbean-infused tune, dressing in a boxer’s warm-up robe, gracing the sauna with Minaj and Speedo-clad men as she doles out her verse. The video concludes with some wetness, as the dancers head to the showers for the finale.


LEO KIHISTORIA Tarehe 30 mwezi8.....


Siku kama ya leo miaka 145 iliyopita, alizaliwa Ernest Rutherford, mtaalamu mkubwa wa fizikia wa nchini Uingereza maarufu kwa jina la baba wa nishati ya nyuklia. Baada ya kuhitimu masomo yake ya awali eneo alikozaliwa, Ernest alielekea katika mji wa kielimu wa Cambridge na kujiunga na chuo kikuu cha mji huo. Kuanzia mwaka 1919 Rutherford alitokea kuwa mhadhiri mwenye kipawa katika uga wa fizikia chuoni hapo, huku akijiunga na jumuiya ya kifalme ya mjini London hapo mwaka 1903. Mwaka 1904, msomi huyo alisambaza kitabu chake alichokipa jina la ‘Shughuli za Mionzi’. Baadaye Ernest Rutherford aliongoza kundi la utafiti katika chuo kikuu cha Manchester, kundi ambalo haraka liliweza kuandaa nadharia mpya kuhusiana na muundo wa atomiki. Mwaka 1908, msomi huyo alitunukiwa zawadi ya Nobel kutokana na shughuli zake hizo na kupata umaarufu mkubwa katika uga huo.

Tarehe 30 Agosti miaka 17 iliyopita, wananchi wa Timor ya Mashariki huko kusini mashariki mwa bara Asia walishiriki katika kura ya maoni na kuchagua kujitenga nchi hiyo na Indonesia. Kisiwa cha Timor ya Mashariki sambamba na visiwa vingine vya Indonesia kilivamiwa na kukaliwa kwa mabavu na wakoloni wa Kireno.Timor Mashariki iliunganishwa na Indonesia mwaka 1976.
Siku kama ya leo miaka 25 iliyopita, Jamhuri ya Azerbaijan ilitangaza uhuru wake kutoka Urusi ya zamani. ardhi ya kaskazini ya Azerbaijan ilikaliwa kwa mabavu na Urusi ya zamani mwaka 1813 kwa mujibu wa mkataba wa Golestan.
Siku kama ya leo mwaka mmoja uliopita winchi lililokuwa limewekwa katika eneo la mashariki ndani ya Msikiti mtakatifu wa Makka lilianguka na kuua idadi kubwa ya mahujaji. Katika tukio hilo lililotokea saa 17.1 kwa wakati wa Makka, mahujaji 107 waliuawa na wengine 238 walijeruhiwa. Mahujaji wengi waliopoteza maisha katika tukio hilo ni kutoka nchi za India, Pakistan, Indonesia na Iran. Serikali ya Saudi Arabia ilitangaza kuwa sababu ya kuanguka winchi hiyo ni upepo na tufani kali iliyovuma mjini Makka

Friday, August 19, 2016

Gwiji wa taarabu Shakila Saidi afariki dunia.....



                                      Muimbaji taarab maarufu nchini Tanzania, Shakila Saidi amefariki dunia Ijumaa nyumbani kwake Mbagala Charambe, jijini Dar es Salaam.
Bi Shakila ambaye alianza kuimba taarab mwaka 1961, alivuma sana katika uwanja wa taarabu mkoani Tanga ambao aliimba katika bendi ya Lucky Star na Black Star. Katika miaka 1980 alijiunga na bendi ya JKT na kujizolea umaarufu mkubwa nchini Tanzania na eneo zima la Afrika Mashariki na Kati. Alistaafu kuimba katika taarabu kwenye bendi hiyo mwaka 1990.Shakila Saidi gwiji katika muziki wa taarabu amefariki.
Atakumbukwa kwa nyimbo zake maarufu ambazo zilizokuwa na ujumbe mzito sana kama "Kitumbiri", "Mapenzi yamepungua" na " Macho yanacheka."
Bi Shakila aliolewa mwaka 1960 akiwa na umri wa miaka 11. Amejaaliwa watoto 13 na wajukuu kadhaa. Atakumbukwa kwa ucheshi wake na mara nyingi alikuwa akialikwa kutumbuiza kwenye sherehe mbali mbali za harusi hasa mjini Dar es Salaam na Tanga.
Mungu ailaza roho yake mahali pema peponi. Ameen.

Watoto waingizwa kwenye jeshi Sudan Kusini.....


Pande zote kwenye mzozo nchini Sudan Kusini zimejihami vikali
Serikali ya Sudan Kusini imewaajiri watoto wavulana kama wanajeshi wakati huu inapojiandaa kwa mzozo mpya, kwa mujibu wa shirika la Associated Press.
Mwanasiasa mmoja mwenye ushawishi anaripotiwa kuongoza shughuli ya kuwaajiri watoto hao, wengine wakitajwa kuwa na umri wa hadi miaka 12 kutoka kijiji kimoja nchini humo.
Nyaraka zinaonyesha kuwa shughuli ya kuwaajiri watoto hao, ilifanyika muda mfupi baada ya baraza la usalama la umoja wa mataifa kuidhinisha azimio wiki moja iliyopita la kutuma wanajeshi 4000 kwenda Sudan Kusini, kuwalinda raia baada ya kuzuka mapigano mapya katika mji mkuu Juba mwezi uliopita.




Mapigano hayo yamekuwa kati ya vikosi watiifu kwa rais Salva Kiir na vile vya makamu wake aliyefutwa kazi Riek Machar ambaye tayari ameikimbia nchi hiyo.
Zaidi ya watu 100,000 walikimbia makwao baada ya mapigano ya mwezi Julai

Shirika la kuwahudumia watoto la umoja wa Mataifa UNICEF linasema kuwa zaidi ya watoto 650 wameajiriwa na makundi yaliyojihami nchini Sudan Kusini tangu mwanzo wa mwaka huu.
UNICEF sasa ina hofu kuwa mzozo huo mpya huenda ukahatarisha maisha ya maelfu ya watoo na kutaka shughuli hiyo ya kuwajiri watoto isitishwe mara moja.
Pia inakadiriwa kuwa watoto 16,000 wameingizwa kwa makundi yaliyojihamia na pia jeshini tangu mzozo nchini Sudan kusini uanze mwezi Disemba mwaka 2013.
Akiongea baada ya kufanya ziara katika maeneo ya Bentiu na Juba nchini Sudan Kusini, mkurugenzi mkuu wa UNICEF Justin Forsyth, alisema kuwa kuna hofu kuwa huenda watoto zaidi wakaingizwa jeshini.

Thursday, August 18, 2016

Harusi za usiku zapigwa marufuku Mombasa............

Sherehe za usikuImage copyrightAFP
Image captionSherehe za usiku
Mamlaka katika mji wa pwani ya Kenya, Mombasa imepiga marufuku harusi za usiku kutokana na sababu za kiusalama.
Kamishna wa eneo hilo Maalim Mohammed anasema kuwa hatua hiyo inalenga kuwalinda wakaazi dhidi ya mashambulio ya magenge yanayotumia visu.
Magenge hayo yamekuwa tatizo kubwa kwa wakaazi katika siku za hivi karibuni huku baadhi ya wakaazi wakiripoti kushambuliwa wakati wa mchana .
Maafisa wa polisi wamekuwa wakifanya operesheni za kiusalama huku washukiwa kadhaa wa magenge hayo wakiuawa.
Wakaazi wa pwani hufanya sana harusi za usiku ambazo huendelea kwa takriban siku kadhaa ikiwemo sherehe za usiku.

Wednesday, August 10, 2016

Gigy Money awataja mastaa 6 aliotoka nao kimapenzi....

Gigy Money Jumanne hii aliwaacha mdomo wazi mashabiki wake baada ya kuwataja live kwenye runinga mastaa 6 wakiume aliotoka nao kimapenzi.
Mavoco, Gigy na Hemedy
Video queen huyo ambaye amewai kutamba katika video za mastaa mbalimbali wa bongo, amedai amewai kutoka kimapenzi na AliKiba, Abdu Kiba, Rich Mavoko, Harmonize, Hemed Phd pamoja na mtangazaji wa kipindi cha runinga cha Siz Kitaa cha Clouds TV, Castro Dickson ambaye alidai alikuwa tayari kumzalia mtoto.
“Nilikuwa na Castro mpaka nilikuwa tayari kumzalia,” Gigy Money alikiambia kipindi cha Take One cha Clouds TV. “kwa sababu anajua upendo kwa mtoto, lakini wakaja wanawake wamjini wakakorofisha, lakini hajawai kuniambia kama tumeachana, sijui kama tumeachana,”
Gigy ambaye pia ni mtangazaji wa Choice FM alidai Mama yake mzazi alimzaa nyuma ya mlango wa choo.
Pia alisema kwamba aliwahi kujitoa kimwili katika umri mdogo ilia pate hela ya kuweza kumnusuru mama yake mzazi kulipa deni la mkopo wa Benki.

Waziri wa Afya atoa siku 14 kwa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Mifupa (MOI).....

Waziri wa afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ametoa siku 14 kwa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Mifupa (MOI) kutathmini na kuangalia matatizo yaliyopo ndani ya taasisi hiyo.
Afisa-wa-Muhimbili-2
Waziri Ummy pia ameagiza kambi za upasuaji zirejee na zianze kazi mara moja ifikapo Agosti 13, mwaka huu.
“Kitu kinachonisumbua kichwa kwa sasa ni kuhusiana na kambi za upasuaji, naomba zianze kazi mara moja, wanaoteseka ni wananchi wa hali ya chini maana baada ya kufutwa kambi za upasuaji ikaanzishwa kambi ya upasuaji wa watu wanaolipia,” amesema Waziri Ummy.
Aidha Waziri huyo ameongeza kuwa atakapopatiwa majibu yote yatakayojadiliwa na kutathimini matatizo yote atatumia nafasi hiyo kumteuwa Mkurugenzi mpya wa bodi hiyo kwa kuwa ni muda mrefu imekuwa ikikaimiwa bila ya kuwa na Mkurugenzi wa moja kwa moja.

TAZAMA PICHA ILIYO WATOKA MAPOVU MASHABIKI WA DAIMOND NA ALLY KIBA.....

Katika mitandao ya kijamii Jumatato hii kumezuka mjadala mkubwa baada ya mashabiki wa Diamond Platnumz na AliKiba kuona picha yakutengenezwa inayowaonyesha wawili hao wakipeana mkono.


Hii ndio picha ya kutengeneza.
13938616_1588978917783187_5262821742312074077_n
Wachache kati ya mashabiki hao wanaamini picha hiyo ni yakutengenezwa huku wengi wao wanaamini wawili hao kweli wamepatana.
Pia miongoni mwa mashabiki hao waamini endapo wawili hao watapana basi na muziki wao utashuka kutokana na kupoteza ushindani.
Haya ni baadhi ya maoni ya mashabiki hao kutoka katika mitandao ya kijamii.

Francis Michael

Tukubali kuwa hakuna jambo lisilokuwa na mwisho kwa upendo wao wenyewe wameona tukiendelea hivi mpaka lini tutamaliza tofauti zetu kwa kuwa wasanii hawa wote wanapeperusha bendela yetu ya TZ, Nimefurahi sana kusikia hivi tofauti zao zimekwisha nawaomba kama kweli umekwisha wafanye kolabo yao wasanii hawa wawili watuchezeshe sasa turuke.

Glory Shayo

Haitawezekana kamwe coz Diamond ana wivu na nyimbo za King Kibaa hiyo itabaki tu story.

Joseph Salvatory

Haitatokea kumaliza tofauti zao hadi Diamond arudishe ile kolabo aliyo mshilikisha Kiba na Kiba kumfunika Diamond, kwa roho mbaya ya Diamond akaifuta.

Veronica Godluck

Elewa kwamba kuna maisha mengine baada ya muziki, na uwezi jua mungu amepanga nini juu yako, so haina haja ya mabifu chamsingi kila mtu awangalie mashabiki wake wanataka nini. Kumake money ndio kila kitu.

Albert Kariuki Tz

Binafsi nita jihisi vibaya kwa kuwa ule ushindani hautakuwepo na muziki yao ni kama vile ita chuja.
Juma Masifia 
Umesema ukweli wote coz kama hawa mastari wangekuwa wana bifu lazima serikali au baraza lao lingeingilia kati na kupelekana mahakamani siyo daily tunasikia mambo tofauti mengi kwenye media na midomo ya watu kumbe hakuna chochote isipokuwa ushabiki wa watu na media
Haruna Hamisi 
Kama wakiungana muziki nao utakuwa umekwisha kwa Diamond & Ally Kiba kwakuwa sasa hivi upinzani wa wasanii hao tu ni gumzo unafanya kuwapa mafanikio makubwa sana kiukweli sasa hivi muziki wa bongo fleva, kwenye soko wameliteka Diamond & Ali Kiba, yaani tunawaangalia wao tu Kiba katoa nini na Mond katoa nn? Sasa wakiungana muziki kwao hakuna tena, kwa hiyo bifu linachangia muziki kwenda mbali

MAHAKAMA NCHINI KENYA YAHALALISHA KUFANYA MAPENZI NA NDUGU......

Habari hii imeripotiwa na BBC ambapo imesema Mahakama ya juu nchini Kenya imehalalisha ngono baina ya mabinamu kwa sababu inakubalika katika baadhi ya jamii nchini humo.
Hatua hiyo imekuja baada ya Mahakama hiyo kumuachia huru mtu mmoja aliyekuwa amefungwa kwa kosa la kushiriki ngono na binamu yake mwaka wa 2014 kwa sababu sio makosa nchini Kenya. Jaji wa mahakama hiyo James Makau, amesema katika maamuzi yake kuwa kujamiiana kwa maharimu sio haramu nchini Kenya………
>>>’baadhi ya jamii nchini Kenya zinaruhusu sio tu ngono bali hata ndoa baina yao, jamii ya wahindi, waislamu na baadhi ya makabila humuhumu Kenya hukubali ndoa baina ya mabinamu’
Jamaa huyo alikamatwa mwaka 2014 kwa kushiriki ngono na mpenzi wake wa kike ambaye pia ni binamu yake na akahukumiwa kifungo cha miaka 10 gerezani.
Hukumu ya jaji Makau imedai kuwa ………>>>’Kwa ufupi hakuna ushahidi wowote uliotolewa kuthibitisha kuwa ngono baina ya wawili hao ni kinyume cha sheria na kwa sababu hiyo ninaamuru mtu huyo aachiwe huru mara moja’

Sunday, August 7, 2016

Video: 42 wajeruhiwa kwenye show ya Snoop Dogg na Wiz Khalifa.....


Mashabiki 42 wamejeruhiwa kwenye show ya Snoop Dogg na Wiz Khalifa huko Camden, New Jersey.
Snoop-Dogg-and-Wiz-Khalifa-perform-may-2016-billboard-1548
Ajali hiyo ilitokea baada ya uzio unaotengenisha stage na mashabiki kuanguka na kuwafanya watu wa mbele waangukiane.

Kwa mujibu wa Philadelphia Inquirer, watu hao walioumiwa wanatibiwa kwa majereha madogo. Wawili hao wapo kwenye ziara ya pamoja waliyoipa jina Merry Jane Presents Snoop Dogg & Wiz Khalifa: The High Road Tour.

Saturday, August 6, 2016

TAZAMA; PICHA za uzinduzi wa mashindano ya Olimpiki 2016 Brazil.....

Mashindano ya Olimpiki 2016 Ijumaa hii yalizinduliwa rasmi mjini Rio De Jeneiro nchini Brazil na kupambwa na burudani ya tamaduni za nchi hiyo.
36EB96AF00000578-3726239-image-a-193_1470444704006
Pamoja na hivyo ufunguzi wa mashindano hao haukubarikiwa na raia wengi wa Brazil waliojikusanya nje ya uwanja kuandamana kuyapinga.
Wananchi hao walipambana na polisi waliotumia mabomu ya machozi kuwatawanyisha. Ndani ya uwanja huo wa Maracana wenye uwezo wa kuchukua watu 80,000 kulikuwa na viti vitupu kibao. Tazama picha mbalimbali za ufunguzi huo.

36EA4EE500000578-3726239-image-a-26_1470437762551

36EB6E2100000578-3726239-image-a-133_1470441937041

36EB9D0300000578-3726239-image-a-217_1470445477840

36EBA62000000578-3726239-image-a-247_1470447087755

36EBBCCA00000578-3726239-image-a-280_1470449502306

36EBEBE800000578-3726239-image-a-39_1470459539188

36EC2DB400000578-3726239-image-a-294_1470450133016

36EC4A7900000578-3726239-image-a-30_1470456617317

36EC6BBA00000578-3726239-image-a-364_1470455162765

36EC7A5B00000578-3726239-image-a-352_1470455071137

36EC7E9F00000578-3726239-image-a-354_1470455073743

36EC16CD00000578-3726239-image-a-270_1470448870038

36EC71CD00000578-3726239-image-a-359_1470455095301

36EC147D00000578-3726239-image-a-267_1470448859222

36EC286A00000578-3726239-image-a-286_1470449963479

36EC596D00000578-3726239-image-a-346_1470454919880

36EC355000000578-3726239-image-a-3_1470455993609

36EC567500000578-3726239-image-a-337_1470453823628

36EC574900000578-3726239-image-a-351_1470455061750
36ECE7D900000578-3726239-image-a-15_1470472498894

Vifo vya watu 13 kwenye Bar Ufaransa........


Wakati nchi ya Ufaransa ikiwa kwenye ulinzi mkali kutokana na mashambulizi kadhaa ya kigaidi hivi karibuni ikiwemo mauaji ya mchungaji katika mji mdogo karibu na Rouen.
August 6 2016 imeripotiwa kutokea kwa moto kwenye bar moja kaskazini mwa Ufaransa kwenye mji wa Rouen na kusababisha vifo vya watu 13 na kujeruhi wengine sita. 
Vyombo vya habari nchini humo vimeeleza kwamba chanzo cha moto huo  ni mshumaa ambao uliwashwa kwenye birthday party ya mtu binafsi iliyokuwa inafanyika ndani ya bar hiyo.

Friday, August 5, 2016

Mama wa Kardashians apata ajali, familia yake akiwemo......

Kris Jenner ambaye ni mama wa familia ya The Kardashian alipata ajali ya gari karibu na nyumbani kwake huko LA.
t
Aligongana na gari nyingine aina ya Prius wakati akielekea nyumbani kwake. Mtandao wa TMZ umeripoti kuwa anaweza akawa amevunjika mkono. Familia yake akiwemo Kanye West waliwahi kwenye eneo la tukio kuangalia kilichojiri. Tazama picha zaidi.

g

Support_system_Kylie_Jenner_Kanye_West_and_Khloe_Kardashian_were-a

r
h

NEW Video: Kcee – Tinana

Hii ndio Video mpya ya Kcce-Tinana......

TOP 3 ya wachezaji watakaowania tuzo ya mchezaji bora Ulaya, Messi out yatangazwa na UEFA....


Shirikisho la soka barani Ulaya licha ya kuchezesha droo ya mechi za play offs za Ligi ya Mabingwa Ulaya, walitangaza majina matatu ya wachezaji wa waliofanikiwa kuingia katika kinyang’anyiro cha kuwania tuzo ya mchezaji bora barani Ulaya 2015/2016.
B3
UEFA wamewatangaza wachezaji watatu ndio wamefanikiwa kuingia katika TOP 3 ya mwisho kati ya wachezaji 10 waliokuwa wamechaguliwa mwanzoni, Cristiano Ronaldo,Gareth Bale wa Real Madrid na Antoinne Griezman wa Atletico Madrid ndio wamefanikiwa kuingia TOP 3.
UE
Washiriki wengine 7 na point zao walioshindwa kuingia TOP 3
Waandishi wa habari kutoka nchi 55 wanachama wa UEFA wanatarajiwa kupiga kura August 25 2016 kumchagua mchezaji bora wa UEFA kwa msimu wa 2015/2016