Friday, August 5, 2016

TOP 3 ya wachezaji watakaowania tuzo ya mchezaji bora Ulaya, Messi out yatangazwa na UEFA....


Shirikisho la soka barani Ulaya licha ya kuchezesha droo ya mechi za play offs za Ligi ya Mabingwa Ulaya, walitangaza majina matatu ya wachezaji wa waliofanikiwa kuingia katika kinyang’anyiro cha kuwania tuzo ya mchezaji bora barani Ulaya 2015/2016.
B3
UEFA wamewatangaza wachezaji watatu ndio wamefanikiwa kuingia katika TOP 3 ya mwisho kati ya wachezaji 10 waliokuwa wamechaguliwa mwanzoni, Cristiano Ronaldo,Gareth Bale wa Real Madrid na Antoinne Griezman wa Atletico Madrid ndio wamefanikiwa kuingia TOP 3.
UE
Washiriki wengine 7 na point zao walioshindwa kuingia TOP 3
Waandishi wa habari kutoka nchi 55 wanachama wa UEFA wanatarajiwa kupiga kura August 25 2016 kumchagua mchezaji bora wa UEFA kwa msimu wa 2015/2016

No comments:

Post a Comment