Wednesday, August 10, 2016

Waziri wa Afya atoa siku 14 kwa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Mifupa (MOI).....

Waziri wa afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ametoa siku 14 kwa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Mifupa (MOI) kutathmini na kuangalia matatizo yaliyopo ndani ya taasisi hiyo.
Afisa-wa-Muhimbili-2
Waziri Ummy pia ameagiza kambi za upasuaji zirejee na zianze kazi mara moja ifikapo Agosti 13, mwaka huu.
“Kitu kinachonisumbua kichwa kwa sasa ni kuhusiana na kambi za upasuaji, naomba zianze kazi mara moja, wanaoteseka ni wananchi wa hali ya chini maana baada ya kufutwa kambi za upasuaji ikaanzishwa kambi ya upasuaji wa watu wanaolipia,” amesema Waziri Ummy.
Aidha Waziri huyo ameongeza kuwa atakapopatiwa majibu yote yatakayojadiliwa na kutathimini matatizo yote atatumia nafasi hiyo kumteuwa Mkurugenzi mpya wa bodi hiyo kwa kuwa ni muda mrefu imekuwa ikikaimiwa bila ya kuwa na Mkurugenzi wa moja kwa moja.

No comments:

Post a Comment