Wednesday, August 10, 2016

MAHAKAMA NCHINI KENYA YAHALALISHA KUFANYA MAPENZI NA NDUGU......

Habari hii imeripotiwa na BBC ambapo imesema Mahakama ya juu nchini Kenya imehalalisha ngono baina ya mabinamu kwa sababu inakubalika katika baadhi ya jamii nchini humo.
Hatua hiyo imekuja baada ya Mahakama hiyo kumuachia huru mtu mmoja aliyekuwa amefungwa kwa kosa la kushiriki ngono na binamu yake mwaka wa 2014 kwa sababu sio makosa nchini Kenya. Jaji wa mahakama hiyo James Makau, amesema katika maamuzi yake kuwa kujamiiana kwa maharimu sio haramu nchini Kenya………
>>>’baadhi ya jamii nchini Kenya zinaruhusu sio tu ngono bali hata ndoa baina yao, jamii ya wahindi, waislamu na baadhi ya makabila humuhumu Kenya hukubali ndoa baina ya mabinamu’
Jamaa huyo alikamatwa mwaka 2014 kwa kushiriki ngono na mpenzi wake wa kike ambaye pia ni binamu yake na akahukumiwa kifungo cha miaka 10 gerezani.
Hukumu ya jaji Makau imedai kuwa ………>>>’Kwa ufupi hakuna ushahidi wowote uliotolewa kuthibitisha kuwa ngono baina ya wawili hao ni kinyume cha sheria na kwa sababu hiyo ninaamuru mtu huyo aachiwe huru mara moja’

No comments:

Post a Comment