Tuesday, August 30, 2016

LEO KIHISTORIA Tarehe 30 mwezi8.....


Siku kama ya leo miaka 145 iliyopita, alizaliwa Ernest Rutherford, mtaalamu mkubwa wa fizikia wa nchini Uingereza maarufu kwa jina la baba wa nishati ya nyuklia. Baada ya kuhitimu masomo yake ya awali eneo alikozaliwa, Ernest alielekea katika mji wa kielimu wa Cambridge na kujiunga na chuo kikuu cha mji huo. Kuanzia mwaka 1919 Rutherford alitokea kuwa mhadhiri mwenye kipawa katika uga wa fizikia chuoni hapo, huku akijiunga na jumuiya ya kifalme ya mjini London hapo mwaka 1903. Mwaka 1904, msomi huyo alisambaza kitabu chake alichokipa jina la ‘Shughuli za Mionzi’. Baadaye Ernest Rutherford aliongoza kundi la utafiti katika chuo kikuu cha Manchester, kundi ambalo haraka liliweza kuandaa nadharia mpya kuhusiana na muundo wa atomiki. Mwaka 1908, msomi huyo alitunukiwa zawadi ya Nobel kutokana na shughuli zake hizo na kupata umaarufu mkubwa katika uga huo.

Tarehe 30 Agosti miaka 17 iliyopita, wananchi wa Timor ya Mashariki huko kusini mashariki mwa bara Asia walishiriki katika kura ya maoni na kuchagua kujitenga nchi hiyo na Indonesia. Kisiwa cha Timor ya Mashariki sambamba na visiwa vingine vya Indonesia kilivamiwa na kukaliwa kwa mabavu na wakoloni wa Kireno.Timor Mashariki iliunganishwa na Indonesia mwaka 1976.
Siku kama ya leo miaka 25 iliyopita, Jamhuri ya Azerbaijan ilitangaza uhuru wake kutoka Urusi ya zamani. ardhi ya kaskazini ya Azerbaijan ilikaliwa kwa mabavu na Urusi ya zamani mwaka 1813 kwa mujibu wa mkataba wa Golestan.
Siku kama ya leo mwaka mmoja uliopita winchi lililokuwa limewekwa katika eneo la mashariki ndani ya Msikiti mtakatifu wa Makka lilianguka na kuua idadi kubwa ya mahujaji. Katika tukio hilo lililotokea saa 17.1 kwa wakati wa Makka, mahujaji 107 waliuawa na wengine 238 walijeruhiwa. Mahujaji wengi waliopoteza maisha katika tukio hilo ni kutoka nchi za India, Pakistan, Indonesia na Iran. Serikali ya Saudi Arabia ilitangaza kuwa sababu ya kuanguka winchi hiyo ni upepo na tufani kali iliyovuma mjini Makka

No comments:

Post a Comment