Wanafunzi 51 wa shule za msingi na sekondari mkoani Dodoma
wamesitisha masomo baada ya kubainika kuwa wamepewa ujauzito kati ya
kipindi cha mwezi Januari hadi Agosti mwaka huu, na hivyo serikali
mkoani humo imetangaza vita!
Takwimu hizo zimetolewa na Mkuu wa wilaya ya Dodoma, Christina
Mndeme katika ufunguzi wa mafunzo ya ufunguzi wa wasimamizi wa mitihani
manispaa ya Dodoma.
“Inasikitisha sana unapopokea taarifa kwa watoto wa kike kupokea
mimba, sasa hivi kwa wilaya ya Dodoma kwa shule za sekondari mpaka
mwenzi huu wa nane ni mimba 45 kwa shule za sekondari na kwa shule za
msingi ni mimba 6,” alisema.
“Ni suala la kusikitisha na kuumiza na ndio maana tunapambana
kuhakikisha wilaya hii tunatokomeza suala hili na ndio maana tumekuja
kwa kauli mbiu hii ya ‘niache nisome magauni manne.'”
Kuhusu wale waliowapa mimba wanafunzi hao, mkuu huyo wa wilaya alisema wakibainika watakiona cha mtema kuni.
“Kwanza ni kuwakamata wale wote waliohusika kuwapa wanafunzi mimba,
kesi ziko polisi kuna wachache wametoroka tunaendelea kuwafuatilia
lakini nitoe wito kwa wazazi watoe ushirikiano kwa serikali yao
kwasababu kumekuwa na udanganyifu kwa wazazi, hivyo kuwafichia siri wale
waliowapa mimba watoto na kuwafundisha kuwakana waliowapa mimba
watoto.”
No comments:
Post a Comment