Leo katika historia jumapili ya tarehe04/09/2016
Siku kama ya leo miaka 134 iliyopita, mota ya kwanza ya umeme ilitengenezwa. Mvumbuzi na mtengenezaji wa mota hiyo alikuwa Thomas Edison mtaalamu na mtafiti wa Kimarekani. Kwa kutumia mota hiyo ya umeme, Edison alianzisha kiwanda cha umeme katika mji wa New York na wakati huo huo akawa amefanikiwa kudhamini sehemu ya mahitaji ya mwanga katika mji huo. Aidha kumbukumbu za kihistoria zinaonyesha kwamba, mwaka 1879, Edison alikuwa amefanikiwa kuvumbua balbu au glopu.
Na siku kama ya leo miaka 108 iliyopita, alizaliwa mwandishi mashuhuri wa Marekani mwenye asili ya Afrika, Richard Wright. Baada ya mashaka makubwa maishani, Richard Nathaniel Wright alianza kazi ya uandishi akiwa na umri wa miaka 30. Baadhi ya vitabu vyake vinaakisi sehemu ya maisha ya kifukara na ya kuchosha ya Wamarekani wenye asili ya Afrika. Ameandika vitabu vingi kama Black Boy, Native Son, Uncle Tom's Children na The Outsider.
Siku kama ya leo miaka 219 iliyopita, jeshi la Ufaransa lilifanya mapinduzi dhidi ya wapigania Ufalme nchini Ufaransa. Miaka minane baada ya mapinduzi ya kihistoria ya nchi hiyo, kutokana na viongozi wa mapinduzi na serikali yao kutokuwa na utendaji mzuri kwa upande mmoja, na kushindwa jeshi la nchi hiyo katika vita kadhaa na nchi za Ulaya kwa upande wa pili, wananchi wa nchi hiyo waliamua kuwapigia kura ya ndio wafuasi wa mrengo wa Ufalme katika zoezi la uchaguzi wa Bunge. Hata hivyo kwa ombi la viongozi wa mapinduzi akiwemo Napoleone Bonaparte, makamanda wa jeshi walifanya mapinduzi mjini Paris na kuwaondoa katika nyadhifa zao Wabunge 177 wa mrengo wa wapigania Ufalme na kuwabaidisha wengine 65 sambamba na kusimamisha uchapishaji wa magazeti 42.
Siku kama ya leo miaka 148 iliyopita alizaliwa katika familia tajiri, François-René de Chateaubrian, mtaalamu wa fasihi na mwanaharakati wa kisiasa wa nchini Ufaransa. Awali De Chateaubrian alikusudia kuwa pasta wa Kikristo hata hivyo akaamua kujiunga na jeshi la Ufaransa. Alikuwa mpinzani wa mapinduzi ya nchi hiyo na katika njia hiyo akapoteza kaka na dada yake. Baadaye alifanya safari nchini Marekani na kisha Uingereza. Wakati wa kuingia madarakani Napoleon nchini Ufaransa François-René de Chateaubrian alirejea nchini kwake na kumtumikia. Hata hivyo haukupita muda mrefu ambapo alitofautiana na Napoleon na kuwa adui wake mkubwa. baada ya kuingia madarakani ukoo wa kifalme, Chateaubrian alikuwa mwanasiasa na pia waziri, huku akiachana na masuala ya siasa na kujishughulisha na uandishi baada ya kuondolewa mfumo wa kifalme nchini humo hapo mwaka 1830.
No comments:
Post a Comment