Monday, September 5, 2016

Majina mashuhuri zaidi ya watoto.....


MtotoImage copyrightTHINKSTOCK

TJina Noah limeingia kwenye orodha ya majina 10 mashuhuri zaidi kwa kupewa watoto wavulana kwa mara ya kwanza, huku Amelia likisalia kuwa jina ambalo wazazi wengi wanawapa watoto wasichana England na Wales, taasisi ya taifa ya Takwimu Uingereza imeonesha.
Jina Oliver ndio linaloongoza upande wa wavulana, likishikilia nafasi ya kwanza tangu 2013 nalo Amelia likiwa juu kwa wasichana tangu 2011. Watoto walioitwa Oliver mwaka 2015 ni 6,941 na Amelia 5,158.
Maafisa wa ONS waliorodhesha majina kando kwa mujibu wa jinsi jina liliandikwa.
Iwapo majina yanayotamwa kwa njia sawa yangewekwa pamoja, basi orodha hiyo huenda ingelikuwa tofauti kidogo.
Mfano ni jina Muhammad ambalo linashikilia nafasi ya 12 likiwa na watoto 3,730.
Kuna wazazi walioandika jina hilo kama Mohammed (2,332) na wengine kama Mohammad (976). Iwapo majina hayo yangejumlishwa, basi jina hilo lingelikuwa katika 10 bora.
Yalikuwepo majina ya kushangaza. Kwa mfano watoto wavulana 17 na wasichana 15 walipewa jina Baby.
Majuzi, utafiti ulionesha karibu sehemu moja kati ya tano ya wazazi Uingereza wanajutia majina waliyowapa watoto wao.

Rocky Balboa na Apollo CreedImage copyrightALAMY
Image captionRocky Balboa na Apollo Creed

Wavulana 35 walipewa jina Rocky, na 21 wakapewa Apollo, labda kutokana na wahusika wakuu wa filamu ya ndondi Rocky Balboa na Apollo Creed.
Wavulana 15 walipewa jina Blue na wengine 14 wakaitwa Ocean. Na kunao 18 walipewa jina Blu.
Kuna jumla ya wavulana 36 ambao watahitajika kujifunza kuandika na kutamka jina lao, Tymoteusz.

Emilia Clarke anayeigiza kama Daenerys katika Games of ThronesImage copyrightPA
Image captionWasichana watano wameitwa Kaleesi

Upande wa wasichana 280 walipewa jina Arya, mmoja wa wahusika wakuu filamu ya Game of Thrones, na wengine 562 wakaitwa Aria, 33 Ariah, 17 Aaria na sita Aariah, jina ambalo huenda ni moja ila likaandikwa tofauti.
Jina Kaleesi, pia kutoka kwa filamu hiyo, lilipewa wasichana watano.
Jina Princess lilipewa wasichana 72, ikikaribia wavulana 77 walioitwa Prince.

The character Maverick played by Tom Cruise Top GunImage copyrightALAMY
Image captionPerhaps boys called Maverick will grow up to become a Top Gun in whatever they do

Takwimu hizo zinaonesha jina Oliver ndilo maarufu zaidi kwa wavulana maeneo yoteb ya Englandisipokuwa London na West Midlands, ambapo jina Muhammad linaongoza.
Jina Muhammad lilipita Oliver eneo la West Midlands mwaka 2014.

Majina mashuhuri zaidi 2015

Oliver Reed
Image captionJina la marehemu Oliver Reed linasalia kuwa maarufu zaidi kupewa wavulana

  • Oliver 6,941
  • Jack 5,371
  • Harry 5,308
  • George 4,869
  • Jacob 4,850
  • Charlie 4,831
  • Noah 4,148
  • William 4,083
  • Thomas 4,075
  • Oscar 4,066

Majina maarufu kwa wasichana 2015

Amelia Boynton RobinsonImage copyrightEPA
Image captionAmelia Boynton Robinson, mwanaharakati mtetezi wa haki za raia Marekani, alifariki mwaka jana akiwa na umri wa miaka 104

  • Amelia 5,158
  • Olivia 4,853
  • Emily 3,893
  • Isla 3,474
  • Ava 3,414
  • Ella 3,028
  • Jessica 2,937
  • Isabella 2,876
  • Mia 2,842
  • Poppy 2,816


Rihanna tuzo za MTV Video Awards New York Agosti 2016Image copyrightREUTERS
Image captionWasichana kadha pia wamepewa jina la mwanamuziki Rihanna

Wasichana 72 walipewa jina Adele, 39 wakaitwa Paloma, kutokana na mwanamuziki Paloma Faith.
Kulikuwa na wasichana 35 walioitwa Rihanna, na tisa Rhianna.
Majina 50 mashuhuri zaidi ya wavulana na wasichana England na Wales mwaka 2015
WavulanaWasichana
NambariJinaWatotoNambariJinaWatoto
1OLIVER69411AMELIA5158
2JACK53712OLIVIA4853
3HARRY53083EMILY3893
4GEORGE48694ISLA3474
5JACOB48505AVA3414
6CHARLIE48316ELLA3028
7NOAH41487JESSICA2937
8WILLIAM40838ISABELLA2876
9THOMAS40759MIA2842
10OSCAR406610POPPY2816
11JAMES391211SOPHIE2779
12MUHAMMAD373012SOPHIA2744
13HENRY358113LILY2711
14ALFIE354014GRACE2658
15LEO346815EVIE2529
16JOSHUA339416SCARLETT2285
17FREDDIE321917RUBY2215
18ETHAN294018CHLOE2158
19ARCHIE291219ISABELLE2119
20ISAAC282920DAISY2113
21JOSEPH278621FREYA2090
22ALEXANDER275922PHOEBE2081
23SAMUEL270523FLORENCE2053
24DANIEL262224ALICE2006
25LOGAN261025CHARLOTTE1951
26EDWARD259326SIENNA1941
27LUCAS244827MATILDA1774
28MAX240728EVELYN1770
29MOHAMMED233229EVA1753
30BENJAMIN232830MILLIE1673
31MASON226331SOFIA1640
32HARRISON224132LUCY1525
33THEO210333ELSIE1513
34JAKE201334IMOGEN1478
35SEBASTIAN198835LAYLA1428
36FINLEY197836ROSIE1403
37ARTHUR196637MAYA1354
38ADAM190338ESME1340
38DYLAN190339ELIZABETH1338
40RILEY172840LOLA1322
41ZACHARY164441WILLOW1308
42TEDDY143042IVY1275
43DAVID139443ERIN1249
44TOBY136344HOLLY1248
45THEODORE130245EMILIA1243
46ELIJAH129446MOLLY1215
47MATTHEW127947ELLIE1185
48JENSON122348JASMINE1182
49JAYDEN121949ELIZA1171
50HARVEY119050LILLY1146

No comments:

Post a Comment