Monday, September 5, 2016

Korea Kaskazini yarusha makombora mkutano wa G20 ukiendelea China...

Makombora ambayo Korea Kaskazini ililipua hivi karibuniImage copyrightAFP/GETTY IMAGES
Image captionMakombora aina ya Scud ambayo Korea Kaskazini ililipua hivi karibuni
Jeshi la Korea Kusini linasema Korea Kaskazini imerusha makombora matatu ya masafa marefu baharini saa chache baada ya Rais wa Korea Kusini Park Geun-hye kukutana na Rais wa Uchina Xi Jinping pambizoni mwa mkutano mkuu wa nchi 20 zenye zilizostawi zaidi kiuchumi duniani.
Makombora hayo yalirushwa kutoka eneo la Hwangju.
Bi Park ametoa wito wa kuwepo kwa ushirikiano zaidi na Uchina, ambayo ni mshirika wa Korea Kaskazini, kuhusu kile alichosema ni uchokozi wa mara kwa mara wa Pyongyang ambayo imekuwa ikifanya majaribio ya mabomu ya nyuklia na makombora.
Vyombo vya habari Uchina vimesema Xi amesisitiza pingamizi zake dhidi ya kujengwa kwa mfumo wa Marekani wa kujikinga dhidi ya makombora nchini Korea Kusini.
Amesema mpango huo huenda ukazidisha uhasama

No comments:

Post a Comment