Wednesday, May 17, 2017

‘Credit ndiyo ilinifanya kutemana na Navy Kenzo’ – Chin Bees....

Rapa Chin Bees amefunguka sababu zilizomfanya kutemana na kundi la Navy Kenzo kuwa ni kukiuka Mkataba waliokuwa nao kulingana na makubaliano yao na kundi hilo na kumnyima Credit kwenye ngoma alizowasaidia.
Image result for chin bees
Chin Bees
Chinbees amesema alikuwa anafanya kazi kubwa sana kwenye kundi hilo ikiwa kuwaandikia ngoma lakini hawakuwa wanaona mchango wake japo hata kwa kumpa credit.
Tulikuwa sawa tu lakini nikakuta wenzangu wananitumia vibaya kwani ninaandika ngoma nyingi tu lakini hawajawahi ata sema kama zile ngoma tumeandikiwa na mtu flani licha ya mimi kupigana kwa ajili yao“Alisema Chinbees kwenye mahojiano yake na Times FM huku akiendelea kukazia kwa kusema.
Credit ndiyo imenifanya mimi ku breakup na Navy Kenzo“Alisema Chin Bees.
Mkali huyo wa hit ya ‘Pepeta’ alitaja mfano wa ngoma aliyowahi kuandika na ikafanya vizuri kuwa ni ‘Kamatia Chini’ ambapo imewatoa mpaka kimataifa lakin hawajawahi kumpa Credit .
Nimeandika ngoma nyingi tu za Navy Kenzo kama Kamatia chini,Nipendelee,na ngoma nyingine imetoka katikati hapa“Alisema Chin Bees.
Kwa sasa Chinbees amesaini mkataba wa mwaka mmoja na Wanene Entertainment na yupo mbioni kuachia Abum yake mpya.

No comments:

Post a Comment