Msani Izzo Buziness amefunguka na kusema msanii kuwepo kwenye chati za muziki, viewers wengi you tube na idadi kubwa ya followers kwenye mitandao si kipimo cha muziki.
Rapa huyo amesema msanii yeyote hawezi kuringia na kumdharau kwa sababu ana idadi kubwa ya viewers youtube kwa kuwa muziki wake hauangalii vitu hivyo.
“Huu muziki unapelekwa tu, kwamba mtu ukifanya vizuri sehemu fulani wewe ndio mkali au mtu akiwa na flowers wengi instagram ndio noma, kuna watu wapo huko hawajui kama kuna instagram.
“Usifikirie ukikakaa kwenye top ten au top twenty umeua, unaweza kuwa huko na kuna sehemu watu hawakosomi wale hawachenguki na wewe, kwa hiyo huu muziki wetu kuna namna bado, kuna vitu vya msingi vya kutiliwa mkazo,” Izzo amekiambia kipindi cha Ladha 3600 na kuongeza.
“Sawa vitu kama you tube tupo katika ulimwengu huo lakini tukiangalia kwa takwimu katika watanzania milioni 40 ni wangapi wana uwezo wa kupata intaneti. Ni topic tu, au ni vitu vya kutrend watu wanatengeneza basi watu wanaflow navyo lakini kwa uhalisia sidhani kama ipo hivyo,” amesema Izzo.
No comments:
Post a Comment