Wednesday, May 17, 2017

Mtoto mwenye umri mdogo zaidi ahitimu chuo kikuu..

Kijana wa miaka 14 amtoa machozi mama yake mzazi kwa kufanikiwa kuhitimu degree yake akiwa ni kijana mwenye umri mdogo zaidi kuhitimu katika chuo cha Texas Christian University kilichopo Marekani.
Carson Huey ni kijana mdogo zaidi kuwahi kutokea kuhitimu masomo yake ya Phisikia,hesabu na kichina kwa kupata Degree ya masomo hayo siku ya 13 Mei. Carson amesisitiza yeye ni kijana wa kawaida licha ya watu kumuona kama mtu mwenye kipaji maalum.
Mama mzazi wa kijana huyo Claretta hakuficha kuonyesha hisia zake na kudondosha machozi wakati mwanae anatajwa jina lake. Alisikika akimshukuru Mungu huku akisema anaamini ipo siku watoto wake watarudisha fadhila kwa jamii yao.

No comments:

Post a Comment