Wednesday, May 17, 2017

Hali ya ulinzi na usalama wa mpaka yetu ni shwari – Serikali.....

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt Hussein Mwinyi amesema vyombo vya ulinzi na usalama kwa kushirikiana na vile vya nchi jirani vimekuwa katika hali ya tahadhari kufuatilia matishio ya ugaidi wa Kimataifa.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe.Dkt Hussein Mwinyi akisoma hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara yake
Waziri Mwinyi ametoa kauli hiyo ambapo akiwasilisha Bajeti ya wizara ya ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa kwa mwaka wa fedha 2017/ 2018 ambapo amesema kuwa hali ya ulinzi na usalama ni shwari.
“Hali ya ulinzi, usalama wa mpaka yetu kwa ujumla ni shwari, baadhi ya maeneo ya ukanda wa Afrika Mashariki, maziwa makuu na Pembezoni ya Afrika ikiwa ni pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Burundi, Somalia na Sudani Kusini,” alisema Dkt Mwinyi.
“Aidha uwepo wa matishio ya ugaidi wa kimataifa umelazimu vyombo vya ulizni na usalama kwa kushirikiana na nchi jirani na raia wake kuendelea kuwa na tahadhari na umakini, endapo kutajitokeza dalili yoyote inayotishia usalama, hatua stahiki ziweze kuchukuliwa haraka iwezekanavyo .”

No comments:

Post a Comment