Wednesday, May 17, 2017

Muziki ni biashara, taarabu ikifanya vizuri naimba – Dogo Janja....

Msanii wa muziki kutoka Tip Top Connection, Dogo Janja amedai yeye ni mfanyabiashara kwenye muziki hivyo anafanya muziki wowote ambao anaona unafanya vizuri sokoni kwa muda huo.
Image result for dogo janja
Dogo Janja
Rapa huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo Kidebe, amedai soko la muziki wa Bongo halihitaji msanii ambaye anafanya muziki wa aina moja kwa muda mrefu bila kubadilika.
“Najitahidi nifanye muziki mkubwa kuonyesha nimekuwa, muziki ninaofanya ni kama unaofanywa na King Kiki,” Dogo Janja alikiambia kipindi cha Ladha 3600 cha EFM. “Naboresha video zangu na kufanya kazi itakayoacha alama hata kama sipo. Mimi nimfanya biashara usishangae leo hii nikiambiwa taarabu inauza mimi nikafumua dude,
Rapa huyo amewataka mashabiki wa muziki wake kukaa mkao wa kula kwaajili ya ujio wake mpya ambapo amedai atakuwa tofauti kama watu walivyomzoea.

No comments:

Post a Comment