Wednesday, May 17, 2017

Davido amnusuru shabiki wake kifo...

Baada ya wiki kadhaa kusambaa kwa video zikionesha shabiki wa mwanauziki Davido kutishia kujiua endapo hatamuona msanii huyo siku ya birtday yake hatimake hit maker ya “if” ameamua kuokoa maisha ya mtu huyo.
Shabiki huyo alipost video na huku akisema kama hatamuona Davido ifikapo Agosti 13 basi hana budi kujiua. Baada ya video hiyo kusambaa hatimaye Davido amekubali kumuona shabiki yake huyo aliopo Nigeria, katika siku hiyo ya kuzaliwa kwake.
Davido amemuhakikishia shabiki huyo kuwa asiwe na shaka atakuwepo katika siku hyo muhimu kwake. Shabiki huyo alisema tangu mwaka 2014 aljaribu kumtumia ujumbe msanii huyo lakini hakufanikiwa kujibiwa hivyo mwaka huu ameamua ni kheri atumie njia hiyo kuonyesha mapenzi ya dhati kwa msanii huyo.


No comments:

Post a Comment