MKUU wa Wilaya ya Kahama, Fadhili Nkulu amewatia mbaroni maofisa afya wa halmashauri ya mji wa Kahama kwa tuhuma za kuacha uchafu katika barabara kuu ya mji wa Kahama ya kwenda katika nchini za jirani za Rwanda na Burundi zikitoa harufu mbaya.
Maofisa walioswekwa ndani ni Johanes Mwebesya na mtendaji wa kata ya Nyasumbi Enocent Kapeli wanaotuhumiwa kuacha wananchi wakitupa taka katika eneo lisilostahili eneo lililopo mwanzo mwa barabara kuu ya kuingia katika mji wa Kahama eneo la Phatom.
Awali mkuu huyo wa wilaya alipita eneo la phatom akielekea halmashauri ya Ushetu kwa ajili ya ziara ya kikazi ya kawaida ndipo aliona rundo la uchafu katika barabara hiyo kuu ya kuingia Kahama Mjini, jambo ambalo alieleza linaleta sura mbaya kwa mji wa Kahama.
Alitoa maagizo kabla ya kuondoka kwenda Halmashauri ya Ushetu mbele ya Mkurungezi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama, Anderson Msumba pamoja na Mtendaji wa kata hiyo na Ofisa Afya wa kata hiyo kuwa akirudi kutoka Ushetu akute uchafu huo umeondolewa hapo haraka jambo ambalo halikutekelezeka.
No comments:
Post a Comment