Wednesday, July 27, 2016

Rapper Chemical adai shule imekwamisha kutoka kwa video yake na Fid Q na Cliff Mitindo

Rapper wa kike Bongo mwenye swagga za hatari Chemical ametaja sababu iliyochelewesha kufanyika kwa video ya wimbo wake ‘Hero’ aliwashirikisha Fid Q na Cliff Mitindo.


Mapema mwezi Mei mmoja kati ya viongozi wa Kazi kwanza wanaomsimamia Chemical waliahidi kuachia video ya wimbo huo kabla ya mwezi huo wa tano kumalizika.
Akiongea na Bongo5, Chemical amesema ugumu wa kupatikana wasanii wote wa tatu walioshiriki kwenye wimbo huo ndiyo umechangia kuchelewa kufanyika kwa video hiyo.
“Huo wimbo tumefanya watu watatu, imekuwa ngumu kukutana wote kwa pamoja. Shule ilileta ugumu kidogo kutokana nilikuwa kwenye mitihani ndio maana kuna vitu vingine nikashindwa kuvifanya,” amesema Chemical.
“Kwa sasa tumeiweka kama pending fulani hivi ila kuna baadhi ya vitu tunavifuatilia vikikamilika tutaanza kushoot,” ameongeza.

No comments:

Post a Comment