Friday, July 22, 2016

Kikwete ampa changamoto Rais Magufuli

Jakaya Kikwete, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM ambaye muda wake unakaribia kuisha amemjulisha mwenyekiti mtarajiwa wa chama hicho Rais Dkt John Magufuli kwa kumweleza kuwa uenyekiti sio lelemama akidai kuwa wajumbe wasipoelewa wanachokitaka, wanakuwa wakali.
magufuli_
Ametoa kauli hiyo leo katika ufunguzi wa mkutano mkuu wa Halmashauri kuu ya chama hicho ambapo kikao hicho kilikuwa na agenda moja tu kupitisha jina la mwenyekiti litakalopelekwa katika mkutano mkuu kwa lengo la kupigiwa kura.
“Tunasema kikao kama hiki hatumwi mtoto tunakuja wenyewe kikao cha leo ni kikao cha kihistoria, kwa maana mbili kwanza ni kikao changu cha mwisho, nikija kwenye NEC ni pale mtakapoliaka lakini tulikubaliana kwamba wazee hao wameishatumikia vya kutosha na tuwaache wapumzike utaratibu wa hapo nyuma ukimaliza uenyekiti unakuwa mjumbe wa kudumu wa kamati kuu na halmashauri kuu,” alisema.
Aliongeza kwa kusema, “Tukaona hatuwezi kuwaita kila siku lakini tunawatengenezea baraza la wazee ambalo ni baraza la ushauri kimsingi linahitajika kwa jambo muhimu sana lakini nilijadiliwa nikaambiwa JK hataki wazee lakini nikasema huo ni uamuzi wa busara kabisa,” aliongeza.
“Na maadam CCM haikuvunjika mwaka jana haitavunjika tena, maana mafisi yalikaa hapa yanasubiri mkono udondoke lakini haukudondoka na maadam haukudondoka mwaka jana CCM haidondoki.”
Kikwete amesema wajumbe hao wanakuwa wakali kwa kuwa wanataka mambo ndani ya chama yaende vizuri ili nao ndani ya chama waweze kujivunia.
CHANZO: MWANAHALIS

No comments:

Post a Comment