Sunday, July 24, 2016

Teknolojia mpya ya vioo vya smartphone visivyovunjika kwa urahisi (Gorilla glass 5) yaja.




Kuvunjika au kupata nyufa ndio ukarabati nambari moja katika matatizo ya simu aina ya smartphone wakati zinapowasilishwa kwa mafundi ili kufanyiwa marekebisho.Sasa, kampuni ya Corning inayoshughulika na utaalamu kuhusu vioo vya simu inasema imefanikiwa kuunda vioo ambavyo havivunjiki kwa urahisi.
Kampuni ya hiyo imekuwa ikiunda vioo aina ya Gorilla Glass ambavyo hutumiwa katika 70% ya simu nyingi za kisasa zikiwemo Samsung na Apple.Sasa inasema kwa kutumia aina mpya ya vioo hivyo, ambayo inaitwa Gorilla Glass 5, skrini za simu zinaweza kunusurika kwa asilimia 80% wakati zikianguka hata kutoka kwa urefu wa mita 1.6.Majaribio ya simu zenye vioo hivyo yaliyofanywa kuwaonesha wanahabari kuthibitisha na baadhi yazo ziliangushwa mara hadi 20 kwenye sakafu ngumu ya maabara hiyo bila kuvunjika.
Nyingi ya simu huanguka kutoka urefu wa kutoka kiunoni au mabega ya mtu, kwani huwa zimewekwa kibetini, mifuko ya suruale ndefu au wa shati au zikiwa zimeshikiliwa.Watengenezaji wa simu wanasema wataanza kuzinadi simu za Gorilla Screen Glass 5 kwenye miezi michache ijayo.
"Tumekuwa tukifanya kazi kwa karibu na wateja wetu, ambao ni makampuni ya simu na wameonesha kufurahia maendeleo hayo," Meneja mkurugenzi wa kampuni ya Corning John Bayne alisema.
Hata hivyo amesema umadhubuti wa bidhaa zinazouzwa unategemea zaidi watengenezaji binafsi wa simu na kuwa kila kifaa pia kinategemea matumizi na matunzo ya mnunuzi na mtumiaji.Kampuni ya Corning imekuwa ikijihusisha na biashara ya utengenezaji na uuzaji wa bidhaa za vioo tangu 1879, ilipotengeneza glass inayotumika kwenye taa iitwayo Edison lightbulb.
Kufikia mwisho wa 2016, zaidi ya simu 4.5 bilioni zitakuwa zimetengenezwa na kuboreshwa kwa teknolojia hiyo ya Gorilla Glass.

No comments:

Post a Comment