Friday, July 22, 2016

Jamii moja nchini Malawi Jamaa analipwa ili kuwatoa mabinti wa kike usichana


Habari hii imeripotiwa na BBC Swahili kuhusu jamii moja nchini Malawi ambayo haithamini ubikira wa watoto wao wa kike. BBC Swahili wameripoti kuwa katika jamii hiyo wazazi wanamlipa mwanaume kumbikiri binti yao punde tu anapopata hedhi yake ya kwanza.
Jamii hiyo inaamini kwamba kuwa na binti ambaye ni bikira ni mkosi kwa jamii, wazazi na jamii kwa ujumla katika maeneo mengi ya kusini mwa Malawi wamekuwa wakishikilia tamaduni hii kwa miaka na miaka.
bbc 2
Wanaume wanaowabikiri watoto wa kike huchaguliwa na wazazi kuwaondolea mikosi, na huwa ni sherehe kubwa inayomtangulia binti kupelekwa unyagoni kisha kuwatembelea shangazi wake kabla ya kujulishwa kwa ‘fisi’.
Mafisi hulipwa takriban dola 7 ambayo ni kama Tsh 15,324 kwa kila kitendo cha ngono na hao mabinti ambao wengi huwa na kati ya umri wa miaka 11-14. Fisi mmoja katika kijiji cha Nsanje, Eric Aniva ameiambia BBC kuwa hajui kwa kweli amewabikiri wasichana wangapi……
>>>”kwa kweli mimi nimewabikiri zaidi ya wasichana 104, hiyo ndio tamaduni zetu pia hapa mwanamke akifiwa lazima aje kwangu nimuondolee mkosi hata kabla ya kuzikwa kwa mumewe’‘.
bbc 6
Aniva ambaye ana umri wa takriban miaka 40 ana wanawake wawili na watoto 5, anasema kuwa pale anaposhiriki ngono na watoto hao huwa anapewa muda wa siku 3 hivi kumsafisha na kumuondolea mkosi.Kulingana na tamaduni zao, ikiwa mwanamke au binti anakataa asibikiriwe huwa wanaamini kuwa jamaa zao watafuatwa na mikosi na magonjwa.
bbc 4
SOURCE: BBC SWAHILIvoice ktiaa tz.blogsport.com

No comments:

Post a Comment