Tuesday, July 26, 2016

Mr T Touch ndani ya studio yake mpya huku akizungumzia juu yakuachana kwake Nay wamitego....

Mtayarishaji wa zamani wa studio ya Nay wa Mitego ‘Free Nation’ Mr T Touch amefunguka na kuzungumzia mahusiano yake na aliyekuwa bosi wake baada ya wawili hao kudaiwa kuachana vibaya.


Mr T Touch akiwa ndani ya studio yake mpya
Akiongea na Bongo5 Jumanne hii, Mr T Touch amesema ameachana na Nay wa Mitego ili kutengeneza maisha yake binafsi.
“Hakuna ugomvi wowote ila mimi nimeamua kufanya maisha yangu ambayo nahisi ni bora kwangu kwa sababu sisi ni binadamu na kila kwenye mwanzo kuna mwisho ,” alisema T. “Kwa hiyo ni vitu vya kawaida mimi nimetoka Free Nation sio kwa bifu lakini ni kujitetea kwenye maisha yangu, kwa hiyo nimefungua studio mpya na nimewekeza pesa nyingi kwa sababu studio ndio maisha yangu,”
Pia mtayarishaji huyo amesema atafanya kazi na Nay wa Mitego kwa vigezo maalum tofauti na mwazo.
“Siwezi kukataa kufanya kazi na Nay wa Mitego, kama akija tutasaini mkataba alafu kazi itafanyika lakini sio kama zamani hii ni kibiashara zaidi,” alisema Mr T Touch

No comments:

Post a Comment