MAMBO safi baina ya Simba SC na kiungo Shizza Ramadhani Kichuya baada ya kuafikiana kufanya kazi pamoja kwa miaka miwili ijayo.
Winga wa Mtibiwa Sugar ya Morogoro, Shizza amesema amepewa ridhaa na klabu yake, Mtibwa Sugar kufanya mazungumzo na Simba SC.
Kichuya
amebakiza mwaka mmoja katika Mkataba wake na Mtibwa, mabingwa wa Ligi
Kuu ya Vodacom Tanzania Bara mara mbili mfululizo, 1999 na 2000.
Na
akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE leo, Kichuya amesema kwamba
amefanya mazungumzo na uongozi wa Simba SC na kufikia makubaliano ya
kuingia Mkataba wa miaka miwili.
“Nimezungumza
na Simba na tumefikia makubaliano, lakini kusaini bado, nadhani wakati
wowote kuanzia sasa naweza kusaini,”amesema Kichuya ambaye leo alikwenda
pia kuzungumza na kocha Mcameroon wa Simba, Joseph Marius Omog
mazoezini Chuo cha Polisi Kurasini, Dar es Salaam.
“Asubuhi
nilikwenda kwenye mazoezi ya Simba (Kurasini) kwa ajili ya kuzungumza
na kocha Omog, nashukuru amenipokea vizuri na amesema yuko tayari
kufanya na mimi,”amesema.
Kama
atasaini, Kichuya atakuwa mchezaji wa tatu wa Mtibwa kuhamia Simba SC
majira haya baada ya Muzamil Yassin na Mohamed ‘Mo’ Ibrahim, wote
viungo.
No comments:
Post a Comment