Saturday, July 23, 2016

Ummy ataka kipaumbele ujenzi hospitali ya wilaya Gairo

 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
HALIMASHAURI ya Wilaya ya Gairo wametakiwa kuweka kwenye mipango yake na kiwe kipaumbele chao ujenzi wa hospitali ya wilaya.
Hayo yalisema na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati akizindua ujenzi wa wodi ya wazazi inayojengwa kwenye kituo cha Afya mjini hapa inayodhaminiwa na Mbunge Ahmed Shabiby.
Waziri Ummy alisema wodi hiyo ikikamilika itawasaidia akinamama wengi wa halmashauri hiyo pamoja na vijiji vya jirani kufika kituoni hapo kujifungua na kuongeza kuwa suala la uzazi kwa mwanamke ni haki yake ya msingi, hivyo kuwa na wodi yao ni haki yao na kwa afya zao na za watoto wanaojifungua.
Alisisitiza juu ya utekelezwaji wa sera ya afya inayohusu matibabu bure kwa wajawazito, wazee na watoto chini ya miaka mitano.
“Nazikumbusha hospitali na vituo vya afya nchini kuwapa kipaumbele kwa kuwapatia matibabu makundi haya, pia muweke dirisha litakaowahudumia wazee, na hii ndio muhimu mlitekeleze,” alisema.
Kwa upande wa watumishi, Waziri Ummy aliwataka waendelee kufanya kazi kwa uadilifu kwa mujibu wa sheria na taratibu za taaluma zao na kuzingatia viapo vyao kwa kuwahudumia wananchi ili kusiwepo na malalamiko yatakayoleta matatizo miongoni mwao.
“Nakuagiza mkurugenzi wa halmashauri uhakikishe unatatua changamoto za watumishi, ikiwemo kuwalipa posho za sare za kazi, likizo na stahiki zao nyingine watumishi hawa,” alisema.
Awali akisoma taarifa ya wilaya, Mkuu wa wilaya hiyo, Siriel Mchembe alitaja changamoto kubwa kwa upande wa huduma za afya ni kukosekana kwa hospitali ya wilaya, gari la kubeba wagonjwa, upungufu wa watumishi pamoja na kutokuwepo kwa zahanati na vituo vya afya katika kata na vijiji hali inayopelekea wananchi kuzifuata huduma za afya umbali mrefuwww.voicekitaatz.blogspot.com

No comments:

Post a Comment