Sunday, July 24, 2016

THOMAS ULIMWENGU AUMIA GOTI TP MAZEMBE,NA KUWAKOSA MO BEJAIA JUMATANO.......

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Emmanuel Ulimwengu ameumia goti la mguu wa kushoto ambalo litamuweka nje si chini ya wiki mbili tangu sasa.
Uli, maarufu kama Rambo mjini Lubumbashi, yalipo maskani ya klabu yake, TP Mazembe ameumia leo akiichezea klabu yake hiyo katika mchezo wa kirafiki dhidi ya timu B.
Mazembe ipo katika maandalizi ya mwisho ya mchezo wa kwanza wa mzunguko wa pili Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya MO Bejaia ya Algeria- maana yake Ulimwengu ataukosa mchezo huo wa Jumatano Uwanja wa TP Mazembe mjini Lubumbashi.

“Nimeumia goti leo, tulikua na mechi ya kirafiki na timu yetu ndogo,”alisema Ulimwengu akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE kutoka Lubumbashi leo.
Ulimwengu sasa atafanyiwa vipimo kesho ili kujua ameumia kiasi gani na atakuwa nje kwa muda gani- lakini taarifa za awali ni kwamba hatacheza Jumatano dhidi ya MO Bejaia.

No comments:

Post a Comment