Katika siku kama ya leo miaka 69 iliyopita alifariki dunia mvumbuzi wa Kimarekani anayejulikana kama baba wa sekta ya utengenezaji magari wa nchi hiyo Henry Ford. Alizaliwa tarehe 30 Julai 1863 katika familia ya kimaskini na tangu utotoni alikuwa na hamu kubwa ya masuala ya mekaniki. Siku moja Ford aliona gari likitembea barabarani bila ya kuvutwa na farasi na akaamua kutengeneza gari lake mwenyewe. Henry Ford alifanyia majaribio mkokoteni wa kwanza usiotumia farasi akiwa na umri wa miaka 12 tu. Mvumbuzi huyo aliboresha zaidi mkokoteni huo na mwaka 1896 alifanikiwa kutengeneza gari lake la kwanza. Mwaka 1895 alipewa haki ya kutengeneza magari licha ya kwamba watu wengine pia walikuwa wanatengeneza chombo hicho na mwaka 1903 aliasisi kampuni ya magari ya Ford Motor. Ford aliwapiku watengeneza magari wengine kwa kutengeneza magari mengi ya bei rahisi.
Siku kama ya leo mwaka 2012 hitilafu katika mitambo ya kuzalisha umeme nchini india yatokea na kuacha zaidi ya watu milioni 300 bila umeme.
Na siku kama ya leo vilevile mwaka 2003 kampuni ya kutengeneza magari ya ujerumani ''Volkswagen'' yaacha kutengeneza kwa mara ya mwisho gari lao lenye staili ya kizamani ya chura aina ya ''beetle'' ama kwa jina maarufu mgongo wa chura.
No comments:
Post a Comment