Saturday, July 23, 2016

Leo kihistoria jumamosi ya tarehe 23/07/2016


Siku kama ya leo miaka 218 iliyopita, jeshi la Napoleon Bonaparte liliwasili katika mji wa Cairo na mji huo ukakaliwa kijeshi na wavamizi wa Kifaransa na kwa muktadha huo utawala wa silsila ya Mamaliki ukafikia kikomo huko Misri.Bonaparte alielekea Cairo mji mkubwa zaidi wa Misri ambao pia ulikuwa mji mkuu wa utawala wa silsila ya Mamalik baada ya jeshi lake kuikalia kwa mabavu bandari ya Alexandria kwa kutumia zana za kisasa za kivita.

Miaka 22 iliyopita katika siku kama ya leo, Sir Dawda Jawara kiongozi wa zamani wa Gambia aliondolewa madarakani kufuatia mapinduzi ya kijeshi na hivyo kulazimika kuikimbia nchi. Jawara alikuwa Rais wa kwanza wa Gambia. Alihudumu kama Waziri Mkuu wa Gambia kuanzia mwaka 1962 hadi 1970. Kuanzia mwaka 1970 alikuwa Rais wa Gambia hadi alipopinduliwa mwaka 1994. Mwaka 1984 Dawda Jawara alikuwa kiongozi wa kamati ya Umoja wa OIC.

Katika siku kama ya leo miaka 17 iliyopita, aliaga dunia, mfalme Hassan II wa Morocco baada ya kukalia kiti cha usultani kwa miaka 38. Alizaliwa mwaka 1929 na kukalia kiti cha usultani mwaka 1961, yaani miaka mitano baada ya Morocco kupata uhuru. Wakati wa utawala wake, mfalme Hassan II alinusurika kuuawa mara kadhaa. Mfalme Hassan II alikuwa mfalme dikteta ambaye alikuwa akikandamiza na kuzima vikali harakati zote za upinzani jambo ambalo lililalamikiwa sana na wananchi wa Morocco. Baada ya mfalme huyo kuaga dunia, mwanawe Muhammad VI alikaLia kiti cha ufalme wa Morocco akiwa na umri wa miaka 36.

Na siku kama ya leo miaka 9 iliyopita, Mohammed Zahir Shah mfalme wa zamani wa Afghanistan alifariki dunia. Zahir Shah alikuwa mfalme wa mwisho wa Afghanistan ambaye aliiongoza nchi hiyo kwa muda wa miaka 40. Alichukua hatamu za ufalme wa Afghanistan akiwa na umri wa miaka 19 tu akimrithi baba yake aliyeaga dunia

No comments:

Post a Comment