Soka ni mchezo ambao umekuwa kama mkombozi wa vijana wengi waliotokea katika familia za kimasikini, asilimia kubwa ya wanasoka wanaotamba katika soka kwa viwango vya juu wametokea familia za kimasikini, ila hiyo haimaanishi kuwa hakuna wanasoka waliotokea familia za kitajiri.
July 23 naomba nikusogezee Top 5 ya mastaa wa soka waliotokea familia za kitajiri.
1- Andrea Pirlo zaidi ya mara moja amewahi kunukuliwa na vyombo vya habari akisema kuwa hakuwahi kucheza soka kwa ajili ya kupata fedha ili kujikwamua kimaisha, ila aliamua kucheza soka kwa sababu ndio mchezo aliokuwa anaupenda.
2- Gerard Piqué wa FC Barcelona historia yake na shule aliyosoma kwao Hispaniainatosha kujua ni kijana aliyetoka katika familia ya inayojiweza, Pique amesoma shule ambayo hawasomi watoto wanaotokea katika familia za chini, hiyo inatokana na gharama ya ada katika shule hiyo.
3- Robin Van Persie huyu anatajwa kuwa toka yupo mdogo aliamua kuwaambia wazazi wake kuwa anataka kuwa mwanasoka, kitu ambacho hakikuwa kigumu kupata sapoti ya kila kitu kwa familia yake kulingana na kwao kuwa na uwezo, ni mwanasoka ambaye hakuwahi kucheza soka peku kama Luis Suarez.
4- Diego Forlán mshambuliaji huyu wa kimataifa wa Uruguay ambaye amewahi kuzichezea Atletico Madrid na Man United, tangu mtoto aliwahi kuwaambia wazazi wake kutokana na kuwa na kipato waunde mfuko wa kuwasaidia watu wasiojiweza.
5- Ricardo Kaka huyu ndio mbrazil wa mwisho kushinda tuzo ya mchezaji bora wa duniaBallon d’Or 2007 na ndio mchezaji pekee aliyewahi kushinda tuzo hiyo mbele yaRonaldo na Messi, Kaka hakutokea familia ya kimasikini kama ilivyo kwa mbrazil mwenzake Ronaldo de Lima, baba yake alikuwa injinia na kaka zake walikuwa wameshafanikiwa katika soka.
No comments:
Post a Comment