“Ni tofauti na ujambazi tuliouzoea. Tunawashukuru polisi kwa umakini waliouonyesha kwa kipindi chote,” alipongeza Jenerali Mwamunyange na kuongeza: “Tulilazimika kushirikiana ili kuwa na nguvu ya pamoja.”
Mwamunyange aliyasema hayo jana wakati akifunga mafunzo maalumu ya kukabiliana na makosa ya kimtandao ukiwamo ugaidi, dawa za kulevya, uharamia, ujangili na usafirishaji binadamu, yaliyowashirikisha zaidi ya askari 200 wakiwamo wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) na wengine kutoka nchi tisa za Afrika, Ulaya na Amerika.
Alieleza sababu za suala hilo kuchukua muda mrefu tofauti na matukio mengi ya ujambazi yaliyozoeleka.
No comments:
Post a Comment