Saturday, July 23, 2016

Soggy Doggy aelezea alivyorekodi wimbo wake wa kwanza kwa shida,alilipiwa studio na mtangazaji huyu..


Msanii mkongwe wa rap Tanzania Soggy Doggy amefunguka nakuelezea jinsi wasanii wa zamani ikiwemo yeye walivyokuwa wakipata tabu kurekodi ngoma kutokana na uhaba wa pesa.
Kupitia kipindi cha Planet Bongo Soggy alijitolea mfano kuwa yeye ngoma yake ya kwanza kwenye muziki aliyoifanya kwa Master Jay alilipiwa na Misanya Bingi ambaye kipindi hicho alikuwa mtangazaji wa radio One,wakati huo kurekodi ilikuwa ni shilingi elfu kumi tu.
Zamani mambo yalikuwa magumu ,hatukuwa na washikaji wenye mkwanja.Mimi ngoma yangu ya kwanza ya kurekodi studio nzuri ilikuwa kwa MJ ambapo hela ya kurekodi ilikuwa ni elfu na aliitoa Misanya Bingi kwa sababu mimi nilikuwa sina kitu na wanangu walikuwa hawana kitu” alifunguka Soggy Dogg

No comments:

Post a Comment