Saturday, July 23, 2016

Mwili wa dereva wa mbio za magari aliyefariki akikwea mlima Kilimanjaro wawasili


Mwili wa dereva wa mbio za magari wa Afrika Kusini aliyefariki wakati akikwea mlima Kilimanjaro, Gugu Zulu umewasili jijini Johannesburg kwaajili ya mazishi.
13694431_532727163602674_150280811_n
Zulu alifariki wiki hii akipanda mlima huo akiwa pamoja na mke wake na raia wengine wa Afrika Kusini.
Alikuwa sehemu ya timu ya Trek4Mandela iliyoshiriki zoezi hilo kuchangisha fedha kusaidia wasichana maskini. Timu hiyo ilirejea Afrika Kusini usiku wa Jumatano hii.
13671074_629992640496712_1340263080_n
Mwili wake uliwasili jana usiku na taratibu za kutoa heshima ya mwisho na mazishi zinafanywa.

No comments:

Post a Comment