Tuesday, July 26, 2016

Koffi Olomide ahukumiwa kifungo cha miezi 18 jela.....


Mwanamuziki maarufu nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Koffie Olomide, amehukumiwa kifungo cha miezi 18 jela.
CoTRfBAWEAEvS2x
Koffi akiwasili kwenye gereza la Makala, Kinshasa kutumikia kifungo
Hukumu hiyo imekuja baada ya wiki iliyopita kusambaa kwa video inayomuonesha akimpiga teke dancer wake wakati wakiwasili kwenye uwanja wa ndege wa JKIA jijini Nairobi alikokuwa atumbuize Jumamosi iliyopita.
CoTRmOOXgAEtBGY
Tukio la kumpiga teke dancer wake limeteka vichwa vya habari duniani mwishoni mwa mwezi huu
Kufuatia tukio hilo alifukuzwa nchini humo na show yake kusitishwa. Show nyingine aliyokuwa aifanya nchini Zambia ilisitishwa siku chache baadaye.
CoTRihzWEAATy7p
Kwa mujibu wa mtandao wa Voice of Congo, hukumu hiyo imependekezwa na mwanasheria mkuu wa serikali. Staa huyo alikamatwa nyumbani kwake wiki hii.
CoTRp-WWIAARFHi
Japokuwa bado hakujatoka taarifa ya kina, imedaiwa kuwa hukumu hiyo haina faini ikimaanisha kuwa Olomide lazima aende jela

No comments:

Post a Comment