Michael Joseph Jackson (29 Agosti 1958 – 25 Juni 2009) alikuwa mwimbaji, dansa na mburudishaji kutoka nchini Marekani. Hufahamika zaidi kwa jina la kiheshima-utani kama Mfalme wa Pop. Hutambulika kama mburudishaji aliyepata mafanikio zaidi kwa muda wote, na moja kati ya waburudishaji wenye mvuto na athira kubwa katika medani ya muziki. Michango yake katika muziki, dansi na fasheni,[1] na hasa suala la kuanika hadharani maisha yake binafsi, imemfanya awe kioo cha ulimwengu katika tamaduni maarufu kwa ziaidi ya miongo minne .
Akiwa pamoja na ndugu zake, Jackson amefanya uongozi wa uimbaji kwa mara ya kwanza akiwa kama mwanachama mdogo kabisa katika kundi la The Jackson 5 mnamo mwaka wa 1964. Ameanza kazi ya usanii wa kujitegemea kunako mwaka wa 1971. Albamu yake ya mwaka wa 1982 Thriller imebaki kuwa albamu yenye mauzo bora kwa muda wote. Mchango waka katika utengenezaji wa muziki wa video umeinua kutoka katika hali ya kawaida hadi katika hali ya kisanii zaidi: video zake kama vile Billie Jean, Beat It na Thriller inamfanya kuwa msanii Mmarekani Mweusi wa kwanza kupata kupigiwa nyimbo yake sana kwenye MTV. Jackson ameipa umaarufu baadhi ya maunja ya kudansi, kama vile robot na moonwalk. Staili ya muziki wake, staili ya sauti yake na zile koregrafia zilitambulika vizazi kwa vizazi, kirangi na hata katika mipaka ya kitamaduni.
Jackson ni mmoja kati ya wasanii wachache waliowekwa mara mbili kwenye Rock and Roll Hall of Fame. Mafanikio mengine yanajumlisha Guinness World Records (ikiwa ni pamoja Mburudishaji Mwenye Mafanikio kwa Muda Wote), Tuzo za Grammy 15 (ikiwa ni pamoja na ile ya Living Legend Award na ile ya Lifetime Achievement Award), 26 American Music Awards (24 akiwa kama msanii pekee ya kujitegemea, ikiwa ni pamoja na moja kwa ajili ya Msanii wa Karne)—zaidi ya msanii mwingine yeyote— single zake 17 zimeshika nafasi ya kwanza huko nchini Marekani (ikiwa ni pamoja na nne akiwa kama mwanachama wa kina Jackson 5), na inakadiriwa kafanya mauzo ya rekodi zaidi ya milioni 750 dunia nzima,[2] inafanya kuwa miongoni mwa wasanii waliouza rekodi zao vilivyo kwa muda wote na haijawahi kutokea .[3]
Maisha binafsi ya Jackson yamezua utata kwa miaka kadhaa. Kujibadilisha kwa mwonekano wake ilianza kutambulika tangu mwishoni mwa miaka ya 1970 na kuendelea, kwa kubadilisha pua yake, na rangi ya ngozi yake, imesababisha makisio kadha wa kadha katika vyombo vya habari. Mnamo mwaka wa 1993 alishtakiwa kwa kosa la udhalilishaji wa kijinsia kwa mtoto, ingawa hakuna mashtaka yoyote yaliyotolewa dhidi yake. Mnamo mwaka wa 2005 amejaribu kuachana na mashtaka kama yale ya awali. Ameoa mara mbili, kwanza alioa mnamo 1994 na akaja kuoa tena mnamo 1996. Amepata watoto watatu, mmoja alizaliwa kwa mama mwenye kuchukua mimba kwa ajili ya familia fulani.
Jackson amekufa mnamo tar. 25 Juni 2009 kwa kuzidisha kiasi cha dawa wakati anajiandaa na ziara ya tamasha lake la This Is It, ambalo lilitakiwa lianze katikati mwa mwaka wa 2009. Ameripotiwa kwamba alitumia dawa aina ya propofol na lorazepam. Afisa uchunguzi wa vifo wa Wilaya ya Los Angeles ameelezwa kuwa kifo chake ni uuaji wa binadamu, na mashtaka yanakwenda kwa daktari wake binafsi kwa kosa la kuua bila kukusudia. Kifo cha Jackson kimeamsha mihemko ya huzuni ulimwenguni, na huduma ya ukumbusho wake uliofanywa hadharani, ulitangazwa duniani, ulitazamwa na maelfu ya watu moja kwa moja.[4]
No comments:
Post a Comment