Baada
ya mauaji ya Wamarekani weusi wawili juzi ambayo yamepelekea kuuwawa
kwa Polisi watano kwenye mji wa Dallas Marekani kama njia ya kulipa
kisasi, Wanahiphop maarufu kutoka jimbo la California Marekani The Game na Snoop Dogg wameongoza kundi la Wanaume kwenye matembezi ya amani mpaka makao makuu ya Polisi.

Moja ya post za The Game akisema ‘sisi sio Wanyama’
Rapper The Game aliitisha matembezi
hayo kupitia Instagram yake na kusema wanaotakiwa kushiriki kwenye
matembezi hayo ni Wanaume tu, Wanawake na watoto wabaki nyumbani na
kwamba Mwanaume yeyote atakaekuja hatakiwi kuwa na silaha yoyote.

The Game na Snoop Dogg wakiongoza matembezi ya amani kuelekea makao makuu ya Polisi Los Angeles California.
Ni matembezi yaliyokua na kusudi la
kuondoa hofu baada ya mauaji kutokea na kuurudisha umoja na ushirikiano
kati ya Polisi na Wananchi, kuanzisha uhusiano mpya na kuondoa hofu ya
kuwindana baina ya Polisi na raia.

Kwenye hii movement yao iitwayo
H.U.N.T (
Hate Us Not Today) viongozi Snoop Dogg na The Game walikutana na uongozi wa Polisi pamoja na Meya wa Los Angeles Eric Garcetti.
The Game amesema ameguswa kufanya hivyo
sababu ameona hali inavyoelekea ni kwamba Ubinaadamu unaondoka ndio
maana akaamua kutumia ushawishi wake kusaidia kumaliza au kukiondoa
kinachotaka kutokea, sisi sio Wanyama.
No comments:
Post a Comment